sponsor

Slider

  1. 1
  2. 2
  3. 3
  4. 4

T - SHIRT PRINTING


LARGER FORMATING

STICKERS BRANDING | LARGE FORMATING


MIFUKO PRINTING

SMALL FORMATING

WEDDING | KITCHEN PART | SEND OFF | INVITATION CARDS

POSTERS | CARTOON | PHOTO PRINTING

» » » MSIFUMBIE MACHO UKATILI WA KIJINSIA
LINK CLASSIC

UNGANA NA 
LINK CLASSIC
KILA SIKU KWA HABARI 

WANANCHI wametakiwa kuacha kufumbia macho suala la ukatili wa jinsia na kujenga tabia ya kuripoti katika vyombo vya dola inapotokea.


Hayo yalisemwa   Dar es Salaam na Janeth Biseki ambaye ni mwanachama wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), wakati wa uzinduzi wa vibanda vya filamu za elimu kuhusu ukatili wa jinsia kwenye kilele cha maadhimisho ya siku 16 za kupinga unyanyasaji na ukatili wa jinsia.

Alisema matukio ya unyanyasaji na ukatili wa jinsia hususan kwa watoto na wanawake yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku kutokana na watu katika jamii kushindwa kuyaripoti katika vyombo husika ikiwa ni pamoja na madawati na asasi mbalimbali zinazohusika na utetezi  ili kutafutiwa ufumbuzi.

“Katika maeneo mengi ambayo TGNP imekuwa ikipita tumekuwa tukikumbana na changamoto ya wananchi kuwa waoga wa kuripoti matukio ya ukatili wa jinsia.

“Kutokana na hali hiyo ndiyo maana TGNP tumeamua kuandaa vibanda vya filamu kama sehemu ya kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa jinsia ambako hizi video za makala zitakuwa na dhima ya kupinga ukatili kwa lengo la kuelimisha na kuibua mijadala katika jamii kuhusiana na vitendo vya ukatili,” alisema.

Aliwataka wananchi kushirikiana na mashirika na asasi za kupinga ukatili wa jinsia kwa kila mmoja kumchunga mwenzake  kuhakikisha vitendo vya ukatili vinakuwa historia nchini.


Asante sana kwa kutembelea Website hii Mungu akubariki sana



Karibuni sana

LINK CLASSIC

LIKE PAGE ZETU 



"KWA HABARI ZAIDI"

BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI

CODE HAPA

«
Next
MACHINGA SASA KUTUMIA VIWANJA VYA SABASABA
»
Previous
RWANDA KUFANYA UCHAGUZI WA RAIS AGOSTI, 2017
Pages 22123456 »

No comments:

Leave a Reply