Wizara ya Maji na Umwagiliaji yaanza kutekeleza Agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufuli la kufikisha huduma ya maji katika eneo linalojengwa mji wa Serikali, Ihumwa Mjini Dodoma kwa kuanza kuchimba visima virefu vyenye uwezo wa kuzalisha mita za ukubwa 600 kwa siku.
Akizungumza wakati wa Ziara yakukagua maendeleo ya utekelezaji wa agizo hilo, Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi, Isack Kamwelwe amesema kuwa maji mengine yatachukuliwa kutoka katika matenki ya Maili mbili ambapo maji yanayozalishwa kutoka katika chanzo cha Makutopora ni lita milioni 71 wakati mahitaji ni lita milioni 46 kwa siku.
Akifafanua Mhandisi Kamwele amesema kuwa kutokana na kuwepo kwa ziada ya maji katika matenki ya Maili mbili mjini humo wataweka mtandao wa mabomba kutoka katika eneo hilo hadi Ihumwa unakojengwa mji wa Serikali ili kuharakisha shughuli za ujenzi wa mji huo.
“Kiwango cha maji kinachosukumwa ni lita milioni 61 tu kati ya milioni 71 tunazozalisha hali inayopelekea tuwe na maji ya ziada ambayo yatasaidia upatikanaji wa maji ya uhakika hapa Dodoma ambapo ndio Makao Makuu ya Nchi,” alisisitiza Mhandisi Kamwelwe.
Aliongeza kuwa moja ya mikakati ya Wizara yake kupitia Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dodoma (DUWASA) ni kuongeza visima virefu katika eneo la Mtumba ambapo visima vingine tayari vimechimbwa tangu mwaka jana ili kukidhi mahitaji ya maji katika Mji huo ambayo ni takribani lita milioni mbili na laki sita.
Aidha Mhandisi Kamwelwe alisema mradi huo unatarajiwa kukamilika ndani ya kipindi kisichozidi miezi mitatu tangu sasa.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge amesema anaridhishwa na hatua zinazochukuliwa na Wizara hiyo kupitia DUWASA katika kuhakikisha kuwa mji wa Dodoma unakuwa na maji ya uhakika yatakayochochea ujenzi wa uchumi wa viwanda na uwekezaji kwa ujumla.
Mradi wa Kufikisha maji katika mji wa Serikali ni moja ya Maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyoyatoa hivi karibuni kwa Wizara hiyo, pamoja na Wizara ya Nishati kuhakikisha kuwa miundo mbinu ya umeme inawekwa katika eneo hilo.
KWA HABARI ZAIDI
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
Hello,
ReplyDeleteHii ni kuwajulisha kwa ujumla kwamba Mheshimiwa John Kerry Jemmy, mkopeshaji binafsi, ana fursa ya kifedha kwa mtu yeyote anayehitaji msaada wa kifedha kwa wanafunzi, mikopo ya kibiashara, mikopo ya uwekezaji, uimarishaji wa madeni na mengi zaidi. Umekataliwa na mabenki na mashirika mengine ya kifedha? Usione tena, kwa sababu tuko hapa kwa matatizo yako yote ya kifedha, tunatoa mikopo kwa kiwango cha 2% kwa watu binafsi na makampuni katika hali wazi na inayoeleweka. Hakuna kuangalia hundi ya mikopo, 100% ya uhakika. Wasiliana nasi leo na utakuwa na furaha kufanya hivyo kwa sababu tuko hapa kutimiza tatizo lako lote na historia ya kifedha.
Tutumie barua pepe kwa: (creditcashexpress8@gmail.com)