UNGANA
NA
LINK CLASSIC
KILA
SIKU KWA HABARI MPYA
Wanaume wengi wanapofikia hatua ya kuoa si kwamba wanakurupuka tu na kuoa mwanamke yeyote mwenye sura nzuri, bali huchukua muda wao mwingi kuchunguza mambo mengi juu ya wake ambao wanadhani kwamba wanaweza kuwa pamoja kwa kipindi chote cha maisha.
Wanawake wengi wanajisahau na kudhani kwamba kitu kinachoweza kuwafanya wakapata wachumba ni uzuri hivyo kupoteza muda wao kujichubua na kujiremba ili wawavutie wanaume bila kujua kwamba kuolewa ni zaidi ya uzuri.
MWEYE MAPENZI YA KWELI
Lengo kubwa la mwanaume kuoa ni kutaka kupata mapenzi ya kweli kutoka kwa mwanamke na ikiwezekana waweze kupata watoto ambapo watoto ndio wamekuwa furaha ya ndoa.
Wapo wanawake wengine ambao wanonesha wazi kutokuwa na mapenzi ya kweli bali wanakuwa na mapenzi ya kuzuga. Wanachotaka wao aidha kupata umaarufu tu kwamba yuko na mtu fulani ama kuweza kupata pesa alizonazo mwanaume lakini sio kwamba ana mapenzi ya dhati kutoka moyoni mwake.
WENYE TABIA NZURI
Tabia njema ndio silaha ya maisha, ukiwa na tabia nzuri kila mtu atakupenda, hiyo ni katika maisha ya kawaida. Lakini linapokuja suala na kuoa, tabia inakuwa kitu cha awali sana kungaliwa na hiyo inaweza kuwa na ukweli kwa sababu wapo wasichana wazuri wenye mvuto wa aina yake na maumbile mazuri, lakini wanakosa wanaume wa kuwaoa, ukiuliza kwani utaambiwa anatabia mbaya.
WENYE UCHU NA MAENDELEO
Hivi karibuni kumekuwepo na mabadiliko ya aina yake kwa wanaume, wengi sasa hivi hawapendi kabisa kuoa mwanamke ambaye hana kazi yaani ‘golikipa’. Kama atakuwa hana kazi basi awe na uchu wa maendeleo kwa kujituma kufanya kazi mbalimbali za kimaendeleo kama vile kilimo kwa wale walio vijijini na biashara ndogondogo kwa wale ambao wako mijijini na hata vijijini.
WASIOPENDA MAKUU
Kuna wanawake wengine wanakuwa na tabia za ajabu sana kiasi kwamba yaweza kuwa kero kwa wanaume. Wapo wanawake ambao wanapenda makuu bila kujali hali halisi ilivyo. Kuna wanawake naweza kusema wana tamaa, kila wikiendi utamsikia “leo tunakwenda wapi dear?” Akimuona rafiki yake kanunua simu ya laki tatu na yeye utamsikia akisema, ‘na mimi naomba uninunulie simu kama ya Grace’.
Asante sana kwa kutembelea
Website hii Mungu akubariki sana
Karibuni sana
LINK CLASSIC
LIKE PAGE ZETU
"KWA
HABARI ZAIDI"
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: