MAOFISA wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wa kituo cha Sirari, mkoani Mara wamelikamata gari aina ya Scania lenye namba za usajili T 291 CBH, mali ya mfanyabiashara wa jijini Mwanza, Charles Nyamaswa likiwa na shehena ya bidhaa za magendo.
Baadhi ya bidhaa hizo ni marobota ya vitenge, majora ya vitambaa, nguo na simu za mkononi, vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya Sh milioni 150.
Bidhaa hizo zilikuwa zikiingizwa nchini kupitia mpaka ya Kogaja Shirati bila ya kulipiwa ushuru.
Akizungumza ofisini kwake jana, Meneja wa Forodha wa kituo cha Sirari mpakani, Narcissius Moshi alisema, Aprili 4 maofisa wao wakiwa doria walipata taarifa ya kuonekana lori hilo likiwa maeneo ya vijiji vya mpaka wa Kogaja Shirati, wilayani Rorya.
Moshi alisema, aliwaagiza maofisa hao walifuatilie ambapo walilikamata likiwa linataka kuingia barabara kuu ya lami kuelekea Mwanza .
“Wahusika wa lori hilo walipoulizwa kuhusiana na bidhaa walizobeba kama zimelipiwa ushuru, walidai kuwa mzigo walio nao haujalipiwa ushuru”, alisema na kuongeza kuwa, baada ya hapo aliwaagiza walikamate lori hilo na kulifikisha kituoni.
Meneja huyo wa TRA Sirari, aliwaasa wafanyabiashara wa mikoa ya Kanda ya Ziwa Mara, Mwanza , Shinyanga , Kagera , Simiyu, Geita na Tabora kuachana na biashara ya magendo badala yake wafuate utaratibu wa forodha na sheria za nchi kwa kulipa kodi bila shuruti.
LINK CLASSIC: Asante sana kwa
kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia
endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya
Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea
website hii
Pia
waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
+255
(0) 652989873 whatsapp
Karibu sana
LINK CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: