UNGANA NA
LINK CLASSIC
KILA SIKU KWA HABARI MPYA
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa
suala la walimu wa serikali kusafiri bure zinaendelea mpaka vyombo vyote vya usafiri kukubali kufanya hivyo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Makonda amesema walimu lazma warahisishiwe maisha katika utendaji wao kazi ikiwa ni kupata usafiri bure katika vyombo vya usafiri vilivyopo jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa katika maombi yake walimu watasafiri bure katika usafiri wa gari moshi za Pungu -Stesheni na Ubungo -Stesheni kwa kutumia vitambulisho ambavyo viko katika utaratibi wa daladala.
Makonda amesema kuwa ameomba Waziri wa Tamisemi juu ya walimu kusafiri bure wa mabasi ya mwendo haraka na baada ya hapo kazi ya kupigania walimu katika vyombo vyote usafiri ili waweze kufundisha watoto na wawe na viwango vya juu vya ufaulu kuzidi mikoa yete nchini.
Aidha amesema kuwa haitakuwa busara suala la walimu kusafiri bure haliwezi likaachwa bila kuwa ufumbuzi kutokana kuamini kuwa walimu wakipata usafiri wanaweza kufika mapema shuleni na kufundisha.
Nae Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa TRL, Masanja Kadogosa amesema kuwa wanaunga mkono jitihada za Rais katika elimu na kama taasisi ya serikali wanachokufanya katika ysafiishaji wa walimu.
Kadogosa amesema kuwa kama kampuni wamechelewa sana kuanza kutoa huduma hiyo na kuongeza kuwa kwa wanafunzi watatumia usafiri huo kwa kulipa sh.100.
Asante sana kwa
kutembelea Website hii Mungu akubariki sana
+255 (0)
652989873 –
Whatsapp / Call
Karibuni sana
LINK CLASSIC
LIKE PAGE ZETU
"KWA
HABARI ZAIDI "
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: