sponsor

Slider

T - SHIRT PRINTING


LARGER FORMATING

STICKERS BRANDING | LARGE FORMATING


MIFUKO PRINTING

SMALL FORMATING

WEDDING | KITCHEN PART | SEND OFF | INVITATION CARDS

POSTERS | CARTOON | PHOTO PRINTING

» » » PROF MUHONGO-SERIKALI ITAJENGA KIWANDA CHA GESI LINDI

UNGANA NA
LINK CLASSIC
KILA SIKU KWA HABARI MPYA

WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amebainisha mikakati ya serikali ya kuwekeza takribani dola bilioni 30 (Sh trilioni 63) kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata gesi kitakachojengwa mkoani Lindi.

Muhongo aliyasema hayo jana kwenye viwanja vya Maonesho ya Kilimo ya Nanenane ya Ngongo, Lindi mara baada ya kumaliza kusoma hotuba ya Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan ya ufunguzi wa maonesho hayo.

Alisema wananchi wa Lindi na Tanzania kwa ujumla wajiandae kwa mapinduzi makubwa ya uchumi katika miaka michache ijayo baada ya serikali kufanya uwekezaji wa kihistoria kama ilivyokuwa wakati Rais wa Kwanza Mwalimu Julius Nyerere alipojenga Reli ya Tazara kwa ushirikiano na mwenzake wa Zambia, Kenneth Kaunda.

“Nataka kuwahakikishia wananchi wa Lindi na Tanzania kwa ujumla kuwa uchumi wetu utakuwa kwa kasi kubwa, tunakwenda kuwekeza kiwanda cha kuchakata gesi ambacho uwekezaji wake hautapungua dola za Marekani bilioni 30. “Kiwanda hiki kitajengwa hapa Lindi na eneo tayari limeshapatikana, hivyo mtegemee mabadiliko makubwa maana sasa Lindi na Mtwara mtabeba uchumi wa nchi hii,” alisema Waziri Muhongo na kuwataka wananchi kuwa watulivu wakati wa utekelezaji wa mradi huo.

Alisema mradi huo unatarajia kuchukua muda mrefu wa wastani wa miezi 40 kwa sababu unahitaji uwekezaji mkubwa wa fedha, ujuzi na uzoefu sambamba na usimamizi wake. Muhongo alisema katika utekelezaji wake, serikali itajenga bomba la kusafirisha gesi lenye urefu wa kilomita 200 kutoka baharini hadi kwenye kiwanda.

“Hii si kazi rahisi, itachukua muda mrefu kwani tunatakiwa kutoa gesi baharini umbali wa kati ya kilomita 100 hadi 200, hadi kiwandani ambako gesi itachakatwa na kuwa kama uji.

Akizungumzia uwekezaji mwingine wa kiwanda cha mbolea kitakachojengwa Kilwa, Waziri Muhongo alisema ujenzi huo utagharimu dola za Marekani bilioni 1.9 (Sh trilioni 4) mpaka kumalizika kwake.

Alisema kiwanda hicho kinatarajia kuzalisha mbolea tani 3,850 kwa siku na kutoa ajira za moja kwa moja kwa Watanzania zaidi ya 5,000.

Asante sana kwa kutembelea Website hii Mungu akubariki sana
+255 (0) 652989873 – Whatsapp / Call

Karibuni sana
LINK CLASSIC

LIKE PAGE ZETU 



"KWA HABARI ZAIDI "

BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI

CODE HAPA

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply