UNGANA
NA
LINK CLASSIC
KILA
SIKU KWA HABARI MPYA
Kufuatia kuboreshwa kwa huduma za usafiri wa reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) na Kampuni ya reli ya Congo (SNCC) ,Kampuni hizi mbili za reli zimekubaliana kwa pamoja kuwatangazia wateja na umma kwa ujumla kuwa kwa sasa huduma hizo zimeboreshwa kwa kiwango kizuri, na hivyo kuwataka wateja wake kutumia reli hizi kuongeza mzigo zaidi wa kusafirisha kati ya Bandari ya Dar es Salaam Tanzania na Jamhuri ya watu wa Congo (DRC).
Viongozi wa reli hizi mbili walikutana Dar es Salaam siku ya tarehe 13 Juni 2016 na kufanya mkutano wa pamoja na wateja wanaosafirisha mizigo mikubwa waliopo Dar es Salaam pamoja na wadau wengine, siku ya tarehe 14 Juni 2016 na kuongelea kwa undani maswala mbalimbali yanayohusu huduma ya usafiri wa reli kati ya Tanzania, Zambia na DRC.
Kwa pamoja, TAZARA na SNCC wamefafanua kuwa wamefanya mabadiliko makubwa katika kuboresha huduma zao hasa katika kipengele cha muda wa kusafirisha mzigo kutoka Lubumbashi na Dar es Salaam kutoka zaidi siku 40 hadi kufikia chini ya siku 10 hivi karibuni. TAZARA yenyewe kwa sasa inasafirisha mzigo kati ya Dar es Salaam na New Kapiri Mposhi kwa wastani wa siku tano.
Waliongeza kuwa, kitendo cha kupungua kwa siku za kusafirisha mizigo pia kimesaidia kuondoa kabisa tatizo lililokuwepo kubwa la wizi wa mizigo ya wateja njiani.
Maboresho haya yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya uongozi yaliyofanywa kwa reli zote mbili ikiwa ni pamoja na hatua zilizochukuliwa na wenye hisa katika kuimarisha reli kwa kuongeza mtaji na vifaa.
Kwa pamoja , TAZARA na SNCC wameelezea masikitiko yao makubwa kuwa pamoja na mzigo mkubwa unaosafirishwa na ukanda wa usafirishaji wa Dar es Salaam (Dar es Salaam Transport Corridor) unaojumuisha nchi za Tanzania, Zambia na DRC kiasi cha asilimia 2% tu ndicho kinachosafirishwa kwa njia ya reli. Hali hii haikubaliki hata kidogo na wamekubaliana kuwa na mikakati ya pamoja ya kuhakikisha kiasi hicho kinaongezeka haraka iwezekanavyo kwa kipindi cha miezi michache ijayo.
Wadau hao wameangalia kwa makini pia jitihada zilizokuwa zinachukuliwa za kuimarisha huduma za reli zao lakini wametaka kuwepo na haja ya kupitia upya bei ya tozo za usafirishaji wa mizigo kwa kuwa usafiri wa reli unatakiwa uwe wa bei nafuu zaidi kuliko usafiri wa barabara.
Wadau hao wametaka reli hizo kuboreshwa kwa kurahisisha operesheni ili kuhakikisha huduma zilizoboreshwa zinatolewa kwa wenye mizigo wa DRC, Zambia na Tanzania, pia kuhakikisha mabehewa ya mizigo yanapatikana mara yanapohitajika.
Kwa hali hii,reli hizi mbili wamekubaliana kwa pamoja kuunganisha nguvu zao katika kuratibu shughuli nzima ikiwa ni pamoja na kupanga mabehewa ya mizigo kwa ushirikiano wa pamoja wa reli ya TAZARA, SNCC na kampuni ya reli ya Zambia (Zambia Railways Limited).
Wadau walioshiriki katika mkutano huo wa pamoja walikuwa ni chama cha wafanya biashara wa Kongo waishio Dar es Salaam (Congolese Business Association), (Zambia Cargo and Logistics Limited), (Tanzania Shipping Agents Association), (Dar es Salaam Corridor Group Limited) na (Tanzania International Container Terminal Services).
Ujumbe wa SNCC uliongozwa na Bw. Romain Kabongo ambaye ni Mkurugenzi wa Biashara na kwa upande wa TAZARA uliongozwa na Injinia Bruno Ching’andu Mkurugenzi Mkuu ambaye pia ndiye aliyeongoza mkutano.
Moja ya treni ya ya mizigo Nchini Zambia
Moja ya treni ya migizo nchini Congo
Asante sana kwa kutembelea
Website hii Mungu akubariki,
+255 (0) 652989873 Whatsapp
/ Call
Karibuni sana
LINK CLASSIC
LIKE
PAGE ZETU
KWA
HABARI ZAIDI
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: