Beki ghali zaidi duniani Virgil van Dijk ameanza kuonyesha thamani yake baada ya kuifungia Liverpool bao la ushindi katika mchezo wake wa kwanza.
Mechi hiyo ya kombe la FA iliyoikutanisha Liverpool na Everton, iliisha kwa matokeo ya bao 2-1 ambapo Van Dijk aliisongesha mbele timu yake baada ya kufunga kwa kichwa akiunganisha kona ya Alex Oxlade-Chamberlain dakika tano kabla mpira haujamalizika.
Beki huyo wa Kiholanzi aliyesajiliwa kwa pauni milioni 75 kutoka Southampton, alicheza kwa kujiamini huku akionyesha kutobabaika na presha ya mechi hiyo ya watani wa jadi.
Liverpool walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza kupitia penalti iliyopigwa na James Milner kunako dakika ya 35 kabla Everton hawajasawazisha dakika ya 67 mfungaji akiwa Gylfi Sigurdsson.
jiunge na group la whatsapp kupata habari haraka bofya hapa
https://chat.whatsapp.com/4kY5fx3UtyA3xYw5uk3NvF
KWA HABARI ZAIDI
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: