sponsor

Slider

T - SHIRT PRINTING


LARGER FORMATING

STICKERS BRANDING | LARGE FORMATING


MIFUKO PRINTING

SMALL FORMATING

WEDDING | KITCHEN PART | SEND OFF | INVITATION CARDS

POSTERS | CARTOON | PHOTO PRINTING

» » » PADRI APIGA MARUFUKU MAHARUSI KUPAKA SHEDO.




UNGANA NA
LINK CLASSIC
KILA SIKU KWA HABARI MPYA


Gazeti la Mtanzania limeripoti kuwa waumini wanawake wanaokwenda kufunga ndoa katika kanisa Katoliki Parokia ya Hananasif Kinondoni, jijini Dar es salaam wamepigwa marufuku kupaka rangi ya mdomo “lipstick”  wakati wa ibada ya misa takatifu ya ndoa.


Gazeti hilo limeongeza kuwa uamuzi huo ulitangazwa juzi jioni na  Paroko wa Parokia ya Hananasif Kinondoni jijini Dar es salaam Padri Gasper Mtengeti, wakati wa ibada ya misa ya kumwombea marehemu Rose Michael iliyofanyika kanisani hapo.

Aidha gazeti hilo limeongeza kuwa kutokana na hali hiyo Padri Mtengeti aliwataka wanawake waache kupaka rangi wakati wa misa takatifu ambapo alitoa sababu tatu zinazotokana na Liturijia ya Ekaristi Takatifu (utaratibuwa uendeshaji wa ibada) chini ya kanisa Katoliki.

Padri Mtengeti alieleza sababu hizo kuwakataza maharusi wa kike kujipaka rangi ya mdomo kuwa rangi hiyo inayopakwa huwa inasalia katika chombo kinachobeba divai ambayo kiimani kwa dhehebu hilo ni damu ya yesu kristu.

Sababu nyingine iliyoelezwa kupitia gazeti hilo ni pamoja na kuwa rangi ya mdomo huwa inachanganyika na damu ya Yesu wakati wanapokunywa kitendo ambacho si chema mbele za Mungu, sababu nyingine ni kuwa rangi hizo hubaki kwenye kitambaa cheupe kinachotumika kufuta kikombe cha hostia baada ya kuguswa na midomo.


Asante sana kwa kutembelea Website hii Mungu akubariki sana

+255 (0) 652989873 – Whatsapp / Call

Karibuni sana
LINK CLASSIC

LIKE PAGE ZETU 



"KWA HABARI ZAIDI "

BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI

CODE HAPA

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply