UNGANA
NA
LINK CLASSIC
KILA
SIKU KWA HABARI MPYA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema kwamba wakuu wa wilaya ambao walikuwa wakifanya kazi hiyo katika maeneo mbalimbali na kuachwa katika uteuzi wake maana yake hawakukidhi vigezo vinavyotakiwa.
Rais Dkt. Magufuli ameyasema hayo alipokuwa akihutubia wakuu wa wilaya aliowateua hivi karibuni ambapo wakuuu wa wilaya 139 waliteuliwa huku wengi wakiachwa katika uteuzi huo na nafasi zao kuzibwa na watu wengine.
Rais Dkt. Magufuli amesema uteuzi huo umezingatia vigezo vya uwajibkaji na uchapaji kazi katika maeneo yao, hivyo walioachwa hawakufanya vizuri inavyotakiwa.
‘’Wakuu wa wilaya tulioachwa hawakufikia vigezo tulivyokuwa tunavitaka pia tumechukua wakurugenzi 22 waliofanya vizuri katika wilaya zao’’- Amesema Rais Dkt. Magufuli.
Aidha Rais amewataka wakuu hao wa wilaya kuchapa kazi na kutumia mamlaka yao vizuri ili kuweza kuweza kutatua kero za wananchi na kuhakikisha haki ili waweze kumuwakilisha vyema katika nafasi hizo.
Asante sana kwa kutembelea
Website hii Mungu akubariki,
+255 (0) 652989873 Whatsapp
/ Call
Karibuni sana
LINK CLASSIC
LIKE
PAGE ZETU
“KWA
HABARI ZAIDI”
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: