UNGANA NA
LINK CLASSIC
KILA SIKU KWA HABARI MPYA
Mimba hatarishi ni ujauzito ambao huatarisha au kutishia afya pamoja na maisha ya mama na mtoto(kichanga)
Nini husababisha mimba kuwa hatarishi?
●Magonjwa au maradhi anayokuwa nayo mama kabla ya ujauzito
Baadhi ya kina mama wana matatizo mengine ya kiafya kabla ya kushika ujauzito. Mfano maradhi ya shinikizo LA damu, kisukari na maambukizi ya VVU. Maradhi hayo hufanya ujauzito kuwa hatarishi
●Unene na kitambi
Kitambi huongeza hatari ya mama mjamzito kupata maradhi ya shinikizo la damu,kisukari,kuzaa watoto wafu, matatizo ya mfumo fahamu pamoja na kujifungua kwa upasuaji na matundu kwenye moyo.
●Mimba yenye zaidi ya mtoto mmoja
Mama mwenye ujauzito wenye watoto mapacha huwa katika hatarishi kubwa kuliko mjamzito ambaye hana pacha. Baadhi ya hatari hizo kwa mama na mtoto ni maradhi ya shinikizo la damu( preeclampsia),uchungu kabla ya muda pamoja na kujifungua njiti. Zaidi ya watoto mapacha huzaliwa kabla ya wiki 37.
●Kushika mimba katika Umri mdogo au mkubwa
Mama anaposhika ujauzito katika umri mdogo (chini ya miaka 17) au katika umri mkubwa (zaidi ya miaka 35) huatarisha afya na maisha yake pamoja na mtoto. Kina mama walioko katika kundi hili wana hatari kubwa ya kupata maradhi ya shinikizo la damu
Mama anaweza kubainika iwapo ana ujauzito hatarishi baada ya kuhudhuria katika clinic za afya ya uzazi na mtoto mapema na mara kwa mara.
Iwapo mama atabainika kuwa na mimba hatarishi atawajibika kuwa chini ya uangalizi wa madaktari bingwa. Hii itasaidia kuhakikisha mama anakuwa salama katika kipindi chote cha ujauzito.
LINK CLASSIC: Asante sana kwa kutembelea Website hii
Mungu akubariki, bila kusahau kuwashirikisha rafiki zako kutembelea website
hii.
+255 (0) 652989873 whatsapp
Karibu sana
LINK
CLASSIC
LIKE PAGE ZETU
"FOR
MORE INFO PLEASE"
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: