UNGANA NA
LINK CLASSIC
KILA SIKU
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema viongozi wakuu wa nchi na washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Rushwa, wamevutiwa na jitihada ambazo Tanzania imezichukua kukabiliana na janga hilo.
Alitoa kauli hiyo wakati akitoa ufafanuzi kuhusu ushiriki wake kwenye Mkutano wa siku moja wa wakuu wa nchi, ulioitishwa kujadili suala la kupambana na rushwa duniani uliofanyika Lancaster House, jijini London, Uingereza.
Waziri Mkuu alisema katika kikao cha kwanza, kilichohudhuriwa na wakuu wa nchi na viongozi wa kitaifa wapatao 20, alipata fursa ya kuelezea jinsi Tanzania ilivyoweza kupambana na rushwa kwa kuzingatia vigezo vikuu vinne.
Waziri Mkuu alivitaja vigezo hivyo kuwa ni kufanya marekebisho ya baadhi ya sheria zinazohusu masuala ya rushwa; uanzishwaji wa mahakama maalum ya mafisadi ambayo inatarajiwa kuanza kazi Julai, mwaka huu; mikakati ya udhibiti wa fedha za miradi ya wananchi na utaratibu wa kubaini wala rushwa kwa kushirikisha jamii ikiwemo kutunza siri za watoa taarifa.
Waziri Mkuu alipata fursa ya kukutana na Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron ambaye mbali na kupongeza juhudi za Serikali ya Rais John Magufuli katika kupambana na rushwa, pia aliahidi kutoa mwaliko ili Tanzania iweze kushiriki kwenye mkutano mwingine wa masuala ya rushwa utakaofanyika Japan, Julai mwaka huu.
LINK CLASSIC: Asante sana kwa
kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia
endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya
Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea
website hii
Pia
waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
+255
(0) 652989873 whatsapp
Karibu sana
LINK CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: