UNGANA NA
LINK CLASSIC
KATIKA KIPENGELE CHA
HOT NEWZ
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ameondoka nchini leo kuelekea Uganda akitokea jijini Arusha.
Rais Magufuli ataungana na viongozi wengine hapo kesho Mei 12 katika sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni ambaye alishinda katika Uchaguzi Mkuu Februari mwaka huu.
Wakati akielekea katika Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) Rais Magufuli amesindikizwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadick pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Felix Ntibenda.

Rais wa Uganda ataapishwa kesho kuongoza taifa hilo baada ya kushinda Uchaguzi Mkuu wa taifa hilo mwezi Februari kwa asilimia 60.75 ya kura zilizohesabiwa.
Wakati huo viongozi wa Chama cha Upinzani cha (FDC) walitangaza kufanya maandamano kuzuia kuapishwa kwa Rais Museveni ambapo walinyimwa kibali na wanajeshi kutanda Jiji la Kampala.
LINK CLASSIC: Asante sana kwa
kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia
endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya
Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea
website hii
Pia
waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
+255
(0) 652989873 whatsapp
Karibu sana
LINK CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA


No comments: