sponsor

Slider

T - SHIRT PRINTING


LARGER FORMATING

STICKERS BRANDING | LARGE FORMATING


MIFUKO PRINTING

SMALL FORMATING

WEDDING | KITCHEN PART | SEND OFF | INVITATION CARDS

POSTERS | CARTOON | PHOTO PRINTING

» » » KWA NINI WANAUME WENGI WALIOKO KWENYE NDOA HUFARIKI MAPEMA NA KUACHA WAKE ZAO?


KWANINI WANAUME WENGI WALIOKO KWENYE NDOA WANAKUFA MAPEMA NA KUWAACHA WAKE ZAO?

UNGANA NA 
LINK CLASSIC 
KILA SIKU KWA HABARI MPYA

1. Umri mdogo wa kikomo cha maisha “life expectancy”
Kama unafahamu hili jambo linaloitwa “life expectancy” utakubaliana na mimi kwamba umri wa mwanaume wa kuishi ni mdogo sana ukilinganisha na mke wake, hususani kusini mwa jangwa la sahara. Kwa hiyo wanawake wanapewa nafasi kubwa ya kuishi muda mrefu kuliko waume zao.

2. Ugumu katika kufunguka
Utakubaliana na mimi kwamba wanaume ni wagumu sana tena sana kufunguka na kushirikisha mambo yao, wao wako tayari wafe na tai shingoni wakijifanya hawaumii au hawasikii shida. Mkiwa na ishu kwenye ndo mkaitwa sehemu muyaongee yeye kamwe hamumpati, anakwambia mambo yetu tutasuluhisha wenyewe wakati ndani yanamla na kummaliza. Na kwa mtaji huu watakufa sana tu

3. Ugumu katika kusamehe
Kusamehe sio tu kwa faida ya anayesamehewa bali pia kwa afya yaw ewe unayesamehe. Mzigo unaotokana na kusamehe hutuumiza sana mioyo yetu, hata kama mara nyingine tunajifanya hatuna shida yeyote. Unaposamehe unaachilia mzigo mkubwa, wanaume wao ni wagumu sna kusamehe. Wako tayari wakubebe moyoni miaka, na tena watakukumbusha uchungu wao kila wanapokuona. Hii inawala sana bila wao kujua.

4. Tabia hatarishi
Wanaume wengi kwenye ndoa ndio wanaoongoza kushiriki tabia hatarishi kama vile ulevi, anasa, ngono holela na hii huwaweka karibu zaidi na jeneza kuliko wake zao waliowaacha nyumbani wakiwadanganya kuwa wako mkutanoni mkoani.

5. Ugumu katika kujali afya
Ni rahisi sana mwanaume akajisikia vibaya lakini asiende hospitalini kuangalia afya, hata pale anapohimizwa kwenda bado anaweza kukwepa au kubisha au hata kusema kuwa ameshakwenda au ameshakunywa dawa kumbe mwongo. Wako pia ambao wanaweza kupewa dawa na wasizitumie.


6. Msongo wa mawazo
Wanaume ndio wabebaji wakubwa wa shehena za msongo wa mawazo “stress” ingawa kwa nje wanajitahisi sana kuonyesha kuwa mambo yako shwari wakati wanatafunwa ndani. Kaulize hospitalini, wanaokufa kwa presha ya kupanda au ya kushuka, stroke, kusimama kwa moyo, kupasuka kwa mishipa ya damu, matatizo ya mifupa, au kuumwa sana kichwa, halafu uliza ni jinsia gani. 


LINK CLASSIC: Asante sana kwa kutembelea Website hii Mungu akubariki, bila kusahau kuwashirikisha rafiki zako kutembelea website hii. 


+255 (0) 652989873 whatsapp


Karibu sana
LINK CLASSIC

LIKE PAGE ZETU 


"FOR MORE INFO PLEASE"

BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI

CODE HAPA

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply