Kabla ya kununua kiwanja chochote ni muhimu kujua ni kwanini unanunua eneo hilo la ardhi. Je ni kwajili ya shughuli za kilimo, nyumba ya kuishi au biashara, kiwanda nakadhalika. Kumbuka kuwa nyumba au ardhi ni hazina kubwa hivyo hakikisha na ni sehemu sahihi ya shughuli yako. Kama ni eneo la kimakazi na unataka kujenga nyumba ya kuishi basi zingatia haya
- Hakikisha muuzaji anatoa hati sahihi kwa kufuata sheria na taratibu za nchi uliyoko.
- Hakikisha ni eneo salama na linalofikika, hapaathiriwi na mafuriko, wala mmomonyoko wa udongo. Pia pasiwe ni karibu na viwanda hatarishi kwa malezi ya watoto
- Pawe karibu na huduma muhimu kama soko, msikiti au kanisa, shule, stendi ya mabasi, hospitali na huduma nyingine muhimu .
- Ni vema pia kuangalia Udongo wa eneo husika kama ni sahihi kwa aina ya shughuli unayotaka kufanya au nyumba unayotaka kujenga.
- Ni vizuri pia kujua kama ni eneo ambalo limepimwa kwa ajili ya makazi ili kuepuka kuvunjiwa yako.
- Je, panamvuto au mwonekano unaotaka wewe? Je kipo ndani ya bajeti yako?
- Vipi hali ya upatikanaji wa maji na umeme katika eneo hilo?
Ukijiridhisha vya kutosha kulingana na matakwa yako ndipo uamue kununua au kuacha.
KWA HABARI ZAIDI
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: