Kalenda tunayo tumia leo imetokana na kalenda ya Juliani ya kirumi. Hapo zamani kalenda hii ilikuwa na miezi kumi tu katika mwaka. Ndio maana Desemba tafsiri yake kwa lugha ni mwezi wa kumi. Baada ya mwezi wa kumi zilibaki siku nyingi za majira ambazo warumi hawakuzijali. Mwezi wa kwanza(machi) ulianza mara baada ya majira mengine kuanza. Miezi yote 10 ilikuwa na siku 29 kulingana na mzunguko wa mwezi.
Mfalme wa pili wa roma Numa Pompilius aliamua kubadilisha kalenda hii kwa kuongeza miezi miwili, Januari na Februari baada ya Desemba ili kumalizia zile siku za majira ambazo hazikuwekwa kwenye kalenda. (Januari ulikuwa mwezi wa 11 na Februari wa 12). Miezi hii miwili iliyo ongezwa ilikuwa na siku 29 kama miezi mingine.
Baada ya kipindi kirefu miezi iliongezwa siku hadi 30 kwa sababu alizo zijua mfalme wa kipindi hicho. Kama hiyo haikutosha baadhi ya miezi iliongezwa siku moja, hivyo kufikia siku 31. mwezi wa siku 31 ulifuatiwa na mwezi wenye siku 30.
Machi 31, Aprili 30 ,may 31, juni 30, julai 31, Agusti 30 na kuendelea.
Baada ya kipindi kingine kirefu, mfalme aliamua kuongeza siku moja katika mwezi Agusti ili kumuenzi Kaisari Agustus, siku hiyo aliitoa katika mwezi wa februari ili asibadilisha urefu wa mwaka. na hiyo ndiyo sababu mwezi huu wa Februari unakuwa na siku 28/29. na pia ndio sababu miezi Julai na Agusti inayo fuatana yote ina siku 31
KWA HABARI ZAIDI
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: