Maamuzi juu ya biashara gani ufanye ni magumu sana na mawazo mengi mazuri ya biashara yanaishia hewani bila utekekelezaji kwa sababu ya kukosa msukumo wa kuanza na kubadili mawazo mazuri kuwa vitendo.
Kuna biashara nyingi zenye faida ambazo zinaweza kufanyika nyuma ya buti ya gari.
Katika mada hii ninaelezea biashara za kufanya katika buti ya gari ambazo kila mwenye gari anaweza kuzifanya kwa mtaji mdogo na bila kuhitaji duka au chumba cha kuuzia.
Kwa wale wenye magari na wanafanya kazi za kuajiriwa biashara hizi zinaweza kuwasaidia kuongeza kipato chao na kuboresha uchumi katika familia zao
Wateja wa Biashara za Kufanya katika Buti ya Gari
Kama ilivyo kwa biashara yoyote ili ufanikiwe ni lazima uwe na bidhaa na masoko,yaani uwe na wateja ambao wanahitaji bidhaa zako au huduma unazotoa. Uwe na wateja wenye njaa au uhitaji kiasi kwamba watakuwa tayari kununua bidhaa zako.
Kwa biashara za aina hii za kufanya nyuma ya buti ya gari, kwa kiasi kikubwa wateja wako ni wafanyakazi wenzako au wateja wa kampuni unalofanyia kazi wakiwemo makampuni shirika na kampuni yako.
Ukiachia wateja wa kazini, unaweza ukauza kwa wanachama wenzako katika vikundi mbalimbali. Watu wengi ni wanachama katika makundi na vyama mbali mbali kama vikundi vya kusaidiana,vikundi vya kikabila na vikundi vya kuinuana kifedha na kibiashara.
Wateja wengine ni washirika katika imani kama makanisani na misikitini na sehemu nyingine za ibada.
Namna ya Kuuza Biashara Nyuma ya Buti ya Gari
Kutegemeana na aina ya bidhaa utakazouza,mpangilio na namna ya uuzaji unaweza kutofautiana. Unaweza kuweka boksi na kuweka bidhaa humo kwajili ya kuwaonesha wateja wako. Kwa bidhaa kama vipodozi au nguo, kabati au boksi linaweza kufaa. Begi au briefcase linaweza kutumika kuoneshea bidhaa zako.
Pia unaweza kutengeneza sanduku la mbao na ukalinakishi vyema kutia mvuto na ukatumia kuoneshea bidhaa zako nyuma ya buti la gari lako. Unapotengeneza boksi ni muhimukutazingatia ukubwa wa buti lako.
Muda wa Kuonesha au Kuuza Bidhaa:
Unaweza kuuza bidhaa zako wakati wa asubuhi kabla ya kazi, wakati wa mapumziko ya chai au chakula cha mchana na jioni watu wanapomaliza kazi.
Unaweza kukaribisha watu na kuwajulisha kwa njia ya ya programu za mtandao lama facebook,twitter na whatsapp. Lakini unaweza kuongea nao moja kwa moja,ana kwa ana.
Barua pepe inaweza kusaidia pia kusambaza ujumbe kwa watu unaowalenga kulingana na bidhaa yenyewe.
Si unajua, huwezi kulenga kila mtu kama unauza nguo za ndani za wanawake mfano au vipodozi vya nywele kwa mfano.
Bidhaa au Huduma Unazoweza Kuuza Kwa Biashara za Kufanya katika Buti ya Gari
Zifutazo ni baadhi tu ya biashara na bidhaa au huduma za kufanya katika gari lako:
1. Nguo
Unaweza kuanzisha biashara ya kuuza nguo katika buti ya gari. Unaweza kuuza ngua mchanganyiko au nguo za aina moja. Mfano ya nguo za aina moja ni kama magauni,nguo za ndani,mashati,suruali,nguo za michezo,mashuka au mabranketi. Nguo mchanganyiko zinahusisha zote zilizotajwa au baadhi yake.
2. Vitafunwa
Wafanyakazi wengi hununua vyakula kwajili ya nyumbani wakitoka kazini. Mfano mkate au mboga mboga ,nyama n.k. Unaweza kuanzisha biashara ya mikate na kuipaki kwenye sanduku nyuma ya buti la gari. Vitafunwa vingine ni keki,maandazi,sambusa na nyama au soseji.
3. Matunda
Unaweza kuuza matunda yasiyoandaliwa au yaliyo andaliwa tayari kwa kuliwa
Matunda yasiyoandaliwa ni kama machungwa asiyomenywa,mananasi,mapapai,maembe. Kama unashamba lako binafsi biashara hii inaweza kukuongezea kipato ambacho ungekosa kama usingeamua kuuza.
Matunda yaliyoandaliwa yahusishwa kumenya matunda na kuyaandaa kwa kuliwa. Mfano ni mchanganyiko wa maembe,papai na tikiti maji ambayo yamekatwa vipande vidogo vidogo na kuwekwa katika vibakuli vyenye vifuniko. Kwajili ya kuongeza ubora na kutunza ni vyema ukaweka katika friji na kisha kutunza katika kitunza ubaridi ambacho unaweza kukiweka katika buti ya gari lako.
4. Bidhaa za Elekroniki
Bidhaa nyingine unazoweza kuuza nyuma katika buti la gari ni zile za eletroniki kama simu,kompyuta mpakato,saa za mkononi,iPad na tableti za aina nyingine kama Samsung au nyinginezo.
5. Juisi za Matunda
Kama ilivyo kwa matunda,unaweza kukamua matunda ya aina moja au mchanganyiko nna kuviweka katika vikopo vyenye mifuniko na kuvipooza katika friji na kisha kuvipaki katika sanduku la kuhifadhi ubaridi ambalo utaliweka nyuma katika buti la gari lako.
6. Bidhaa za Watoto
Wazazi wanawapenda watoto wao na wako tayari kulipia bidhaa kwaajili yao. Hivyo bidhaa za watoto nimojawapo ya zile zinazouza sana. Unaweza kuuza bidhaa za aina moja kama chupi za mkojo (daipa),midoli ya kuchezea,mashati na suruali.
Au unaweza kuamua kuuza bidhaa za watoto za aina moja kama viatu au chupi pekee.
7. Vipodozi
Vipodozi na bidhaa za urembo zina soko kubwa hasa kwa wakinadada na akina mama. Bidhaa kama marashi ya chupa, mafuta na losheni za ngozi na mafuta ya nywele ni baadhi ya bidhaa unazoweza kuuza kwa faida nyumba ya buti ya gari lako.
8. Vito na bidhaa za kuvaa mikononi na shingoni
Bidhaa za kuvaa shingoni na mikononi ni biashara nyingine has a inayowagusa wanawake.
Bidhaa kama cheni za dhahabu,shaba,na madini mengine ya vito vya thamani yanahitajika na yanauzika kwa wingi. Bangili za mitindo tofauti kama plastiki,shaba,silva na madini mengine yanaweza kuwa biashara nzuri nyuma ya gari lako.
9. Mboga mboga na Viungo
Mboga mboga kama karoti,pipili hoho,vitunguu,nyanya chungu na bidhaa nyingine za bustanini kwako au hata kama utazinunua zinaweza kuuzika na kukuongezea kipato katika duka ndani ya gari lako.
10. Urembo wa Kucha na Mikono
Tumezungumzia zaidi bidhaa,lakini kuna huduma pia unazoweza kuzitoa katika gari lako. Urembo wa kucha kama kusawazisha kucha na kupaka rangi za kucha na vidole kama hina na piko ni mojawo ya huduma unazoweza kufanya katika gari lako.
11. Bidhaa za Biashara za Mtandao
Mojawapo ya biashara maarufu zenye faida siku hizi ni biashara ya mtandao,ni biashara za kuuza bidhaa toka makampuni ambayo yanauza na kusambaza bidhaa zake kwa kupitia mtu mmoja mmoja kwa njia ya mdomo.
Wasambazaji ni watu ambao wanatumia bidhaa hizo na wanapata malipo kwa kuwashirikisha wengine na kuwasajili katika biashara. kuna makampuni maka Forever Living Products, Organo Gold na mengine mengi.
Bidhaa hizi ni rahisi kuuza katika buti ya gari na ni rahisi kuwainesha na kuwashirikisha watu wengine kwa njia hii
Mwisho
Japo biashara hizi si za kutegemea sana kama chanzo cha kwanza cha kipato lakini zikifanywa vizuri zinaweza kuongeza kwa kiasi kikubwa kipato chako.
Wataalamu wa uchumi binafsi wanashauri kuwa na vyanzo zaidi ya kimoja vya fedha ili kufanikiwa kifedha na biashara za kufanya katika buti ya gari lako zinaweza zikasimama kama chanzo cha pili cha kipato.
Je wewe unafikiriaje? Kuna biashara nyingine katika mawazo yako ambazo unaweza kufanya katika buti la gari lako? Shiriki nasi kuchangia katika sanduku la maoni hapa chini.
Nakutakieni usomaji mwema na michango katika mada hii na muhimu zaidi kufanya kwa vitendo angalau wazo mojawapo katika haya kumi. Tutaonana tena katika mada nyingine.[:]
KWA HABARI ZAIDI
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: