Awali ya yote inabidi nieleze na kutoa mkazo kuwa biashara za mtandao ni kufanya kazi na watu na kuwafundisha jinsi ya kubadilika na kupata kipato kufikia viwango vya juu. Kitu kikubwa ni kujifunza na kutumia mbinu bora za kujenga timu chini yako.
Ukisha kuwa na kikosi ambacho umekifundisha vizuri, kitafanya kazi na kukufanya uongeze kipato chako kila mwezi. Unaanza na kuwafundisha wale ambao umewasajili binafsi, nao watawafundisha waliowasijili na zoezi hilo kujirudia rudia na hatimaye kupata kikosi bora kinachofanya kazi. Kampuni nyingi za mtandao zinatoa mafunzo na kutoa nyenzo za kusaidia katika kutoa mafunzo.
Sasa ili uweze kupata mafanikio kwenye biashara za mtandao, pitia kwa makini na tekeleza yafuatayo:
Chagua Vizuri Kampuni Yako Ya Mtandao
Kwangu mimi binafsi, hili ni la maana kuliko mengine yote ambayo tutayajadili hapa chini kwa sababu ikiwa utaangukia mikononi mwa kampuni mbovu, haya yote tunayoyajadili kwenye mada hii hayatakusaidia, hata kama utatumia nguvu na mbinu za namna gani. Zingatia yafuatayo katika kuchagua kampuni yako ya kufanya nayo biashara:
1.Sifa Za Kampuni:
Chunguza sifa za mmiliki wa kampuni unayotaka kujiunga nayo na historia ya kampuni kwa ujumla. Kampuni iliyo kwenye biashara hii kwa muda mrefu, itakuwa na uhakika zaidi katika shughuli zake. Chunguza vile vile katika kipindi ambacho kampuni imekuwa ikifanya kazi imekuwa na rekodi gani.
Jee, imewaingiza wanachama kwenye migogoro ya aina yo yote? Kuna wanachama ambao wametajirika na kampuni hiyo? Inakua kibiashaara, imefikia ukomo au inateremka kibiashara? Jiunge kwenye kampuni ambayo majibu yake kwa maswali hayo ni mazuri.
2. Uzuri Wa Bidhaa Au Huduma Za Kampuni:
Mteja ye yote yule atanunua bidhaa ya kampuni au atapenda kupata huduma za kampuni pale tu ambapo amapata sifa kuwa bidhaa za kampuni hiyo au huduma ya kampuni hiyo itamsaidia kuondoa matatizo aliyo nayo na si kinyume cha hilo. Kampuni yenye bidhaa nzuri au huduma nzuri itakupunguzia kazi ya kufanya matangazo au kutoa maelezo badala yake utapata wateja wengi na kupata faida kubwa.
3. Mpango Mzuri Wa Malipo (Good Compensation Plan):
Mpango wa malipo wa kampuni unayofanya nayo kazi ndio utakaosema wewe kama mwanachama utapata kiasi gani kutokana na kazi uliyoifanya. Kwa vile ulijiunga ili upate kipato kizuri, haina maana kujiunga na kampuni ambayo haina mpango mzuri wa malipo. Ni vizuri kujiunga na kampuni ambayo ina mpango wa malipo unaoeleweka kiurahisi na unaotekelezeka.
4. Msaada Wa Mafunzo Na Nyenzo Za Kazi:
Kampuni inayotoa mafunzo ya bure kwa wanachama wake, vipeperushi na vifaa
vingine vya kusaidia kufanya kazi itakusaidia kufikia malengo yako ya kupata kipato kikubwa kwa muda mfupi zaidi. Kampuni iliyo bora itatoa njia nyingi za kutoa msaada, namna nyingi za kuweza kujifunza kuhusu biashara yake, mabango, tovuti binafsi na vitu vingine ili uweze kupanda kiurahisi na kufikia malengo yako.
Ielewe Vizuri Kampuni Yako
Chukua muda wa kutosha kujifunza kuhusu mpango wa malipo wa kampuni yako, kampunii nyingine zina vitu vingi sana ambavyo ungeweza kuvifanya. Ukisha pata undani wa kampuni, amua njia yako utakayofuta katika kufikia malengo yako katika biashara ya kampuni hiyo. Pata ushauri kila mara kutoka kwa watu walio juu yako ili ujue njia walizotumia kufanikiwa katika biashara ya kampuni
Ongoza Timu Yako Vizuri
Wanachama wapya kwenye kampuni wanahitaji msaada kama vile ulivyohitaji wewe wakati unaanza biashara na kampuni hiyo. Hakikisha unatoa muda wa kutosha kuwafundisha kuhusu biashara yenu, washike mkono hadi pale watakapoanza kumudu kuifanya biasharaa hiyo wenyewe. Kumbuka kuwa kufanikiwa kwa walio chini yako ndiyo mafanikio yako. Kusajili wanachama chini yako kisha kuwaacha yatima hakutakusogeza po pote katika biashara yako.
Tumia Vizuri Mtandao
Kwa wakati tulio nao sasa, hakuna chombo bora cha kufanyia matangazo ya biashara yako zaidi ya matumizi ya mtandao (internet). Unaweza kutumia mitandao ya kijamii (social media sites), ukajenga blog au tovuti kwa ajili ya kuitangaza biashara unayofanya.
Mitandao ya kijamii yote mikubwa – Facebook, Google+, Instagram Tweeter n.k. – inaruhusu watu kufungua akaunti bure na kutangaza biashara zao bure kabisa. Baadhi ya mitandao inaruhusu kufungua kurasa za kibiashara, kwa mfano, Fan Page kwenye facebook, ambamo utajenga urafiki na watu mbalimbali ambao wataelewa ni biashara gani unaifanya.
Jee, una mbinu ambazo umezitumia kufanikiwa na biashara za mitandao ambazo hazijatajwa hapa na ungependa kuwafahamisha wasomaji wengine? Usisite kutuandikia.
KWA HABARI ZAIDI
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: