Mafanikio yoyote huanza kwanza na mabadiliko ya fikra na mtazamo katika bongo zetu,yaani kwa kuwa mtu chanya na mwenye shauku,asiyoona mipaka ya kutafuta kila anachokita na asiye kata tamaa katika kufikia kile anachokitumainia kukipata licha ya changamoto nyingi.
Kwanini nataka ubadili fikra na mtazamo wa familia yako?
Sote tunatambua kuwa msingi mkubwa wa malezi ya makuzi yetu hutoka katika familia tunazoishi,hapa ndio kiini cha mambo mengi tunayojifunza toka utotoni,ni jukumu la mzazi,mlezi au mwanafamilia kuhakikisha kuwa anatumia juhudi zake zote katika kuwaelimisha wana familia wake swala la kuwa na fikra chanya nyakati zote,natambua hili siyo jambo rahisi kabisa hata kidogo kutoka na jamii zetu zinavoishi katika mfumo wa imani ya mtazamo tofauti tofauti ulipandwa kwenye akili zao kutoka aidha kwa wazazi,walezi au jamii wanaliyokulia.
Habari njema ni kwamba tunaishi katika ulimwengu ulioendelea mno tofauti na vizazi vyote vilivopita,teknolojia imekua sana,hata kujifunza chochote unachota ni virahisi kupata maarifa katika vitabu,makala,tamthilia,filamu,vipeperushi na mitandao kadha wa kadha,naamini nawe ndugu yangu unanufaika na haya mojawapo kwa kusoma makala mbali mbali toka ndani ya blog hii.Kazi uliyonayo ni kupanda mbegu hii ya maarifa unayojifunza kwa watoto wako ,ndugu,jamaa,rafiki na jamii inayokuzunguka.
Watoto ni watu muhimu sana katika jamii wawezesha wapatia maarifa sahihi wangali wadogo,kumbuka msemo usemao ”samaki mkuje angali mbichi”,ni vyema kuwapika watoto wetu mapema ili wakue katika fikra chanya katika maisha yao,huu utakuwa ni ukombozi mkubwa sana katika taifa letu kwa kupanda mbegu hii muhimu sana,kwa sababu asimilia kubwa ya watu wote tunatoka katika familia mbali mbali,kwa kutoa elimu bora kabisa ya maarifa sahihi kwa watoto wetu unatakuwa ni msaada mkubwa na wenye nguvu kubwa sana tofauti na kujifunza maarifa haya ukubwani.
Tambua pia kuwa Utajiri wa kweli na uhakika huanzia kwenye fikra zetu, vile unavowaza mara kwa mara ndivyo utarajiacho kuvuna ndugu yangu.
Tujitahidi kulea familia zetu katika utofauti na tulivolelewa sisi tulio wengi, tumekua tukiwa bongo zetu zimejazwa imani za hofu,uoga,kushindwa na hali ya kutojiamini.Ukiangalia tumeshindwa kuzitumia fursa nyingi kwa sababu ya kujawa na magonjwa haya,tusiendeleze tena kuilisisha hali hii katika kizazi kijacho kwa sababu tumeutambua ukweli huu ndugu msomaji, kumbuka hata ambao waliokujaza imani hizi halikuwa kosa lao bali walitaka nawe uwe kama wao kwa kukufundisha kwa uaminifu mkubwa yale ambayo waliamini yatakusaidia katika maisha yako,pengine wangeutambua ukweli huu ndo hicho ambacho ungekipata toka kwao.Huna budi sasa nawe kuwa mtiifu katika hili kwa waelimisha wote wanaokuzunguka wakubwa kwa wadogo pia.
Naamini sasa mpenzi msomaji makala hii umejifunza kitu ambacho hakika kitaweza kusaidia jamii yetu kuweza kubadili mtazamo wetu kwa kuwa na fikra chanya iliyotawala katika maisha ya kila siku,kwa sababu fikra hii ina nguvu kubwa sana katika safari yako ya kusaka mafanikio unayoyatamania.Tuujenge msingi huu kwa watoto wetu kwa nguvu zetu zote kwa kuwashirikisha pia kwenye maamuzi na majukumu makubwa kwa madogo katika familia zetu ili kuwajengea uwezo mkubwa wa kuweza kujiongoza vyema kwenye maisha yao baadae bila kuteteleshwa na changamoto nyingi za maisha.
KWA HABARI ZAIDI
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: