Kanuni muhimu za kuwa baba bora na anayejua wajibu wake.
Leo tumekusogezea muhimu kwa wale wanaotaka kuwa akina baba bora.
Leo tunataja mambo matano muhimu ikiwa unataka kuwa baba anayejua wajibu wake kwa watoto wake.Zingatia yafuatayo yatakusaidia kuwa baba bora na sio baba.Kuna utofauti wa baba na baba bora.Tutawaelezea kipindi kijacho
1. Upendo.
Huu ndio wajibu mkuu kuliko wajibu wowote unaoweza kuwa nao kama baba. Anasema kuwapa chakula, malazi, mavazi ili wakue, si kazi ngumu. Kazi ni kumfanya mtoto ajisikie kupendwa, hali ambayo ndiyo itakayofinyanga tabia yake ukubwani. Kipimo cha mafanikio ni ikiwa unaweza kumfanya mwanao ajisikie kupendwa,
2. Kuwa mfano.
Maisha unayoishi yana maana kubwa kwa wanao kuliko maneno unayowaambia. Unachofanya ndicho kinachochukuliwa serious. Ukizoea kuwaadhibu, ndicho wanachojifunza. Ukiwabana sana, hawajifunzi kutushirikisha walivyonavyo. Kama unataka wanao wale chakula bora, anza wewe. Ukitaka wasome, onyesha mfano.
3. Wakumbatie.
Ni bora kuwakumbatia kuliko kuwaadhibu. Kwanza ni njia nyepesi ya kuonyesha upendo. Hiyo haimaanishi hawakosei, maana hata sisi tunakosea. Tunawaadhibuje wao, ikiwa sisi hatungependa kuadhibiwa? Anasema, njia bora ni kuwa mwelewa. Kuvaa viatu vya mwanao. Fikiri nini kingesaidia, jadilini tatizo lilivyo, kuliko kukimbilia kuadhibu. Badala ya kukazania ubaya, onyesha mtu mwema anapaswa kuwaje.
4. Waamini.
Waache wajaribu na washindwe. Onyesha kwamba kukosea ni sahihi vilevile, na kujaribu ni sawa. Usiwafanye waogope kujaribu kitu. Ukifanya hivyo, watakuwa mazezeta. Onyesha kutokuogopa kushindwa wewe mwenyewe, waelewe kushindwa ni sehemu ya majaribio. Ukiwaamini watajiamini.
5. Wape fursa ya kuwa wanavyotaka kuwa.
Usitake unachotaka wewe ndicho wawe wao. Wewe ni wewe, na watoto wanacho wanachopenda wao. Mwache mtoto ajipambanue kwa njia yake. Afanye chaguo lake mwenye, makosa yake mwenyewe, na wewe msaidie kihisia. Cheza michezo yao ya kitoto. Toka nao. Zungumza nao. Wasimulie hadhithi. Fuatilia wanavyovipenda iwe muziki, dansi, na kadhalika.
KWA HABARI ZAIDI
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: