Wakati wa mtihani huwa mgumu kwa watu wengi, hususan Asia mashariki ambapo kuna shinikizo kubwa kwa watu kufaulu.
Licha ya tofuati za kitamaduni, wanafunzi wote wana itikadi na imani zao, iwapo ni kuimba nyimbo kula chakula maalum au hata kuvaa nguo wanaoiona kuwa na bahati kwao.
Hizi ni baadhi ya mbinu zinazotumika kote Asia na wanafunzi kuhakikisha wanafualu kwa ukubwa:
Kula tufaha(apple) kwa siku
Migahawa katika vyuo viku Hong Kong huwapa wanafunzi matufaha na vyakula vinavyotengenezwa kutokana na tufaha wakatimithani ikikaribia.
"Tufaha kichina hutamkwa "ping guo", yaani "salama". Kwahivyo inadhaniwa utapasi mtihani salama," anasema Chong Wang, kutoka Nanjing China.
Epuka kuosha nyelewe
Iwapo umsahau kuoga na zaidi kuosha nyele katika harakati zako za kutwalii, usiwe na wasiwasi, huko Korea kusini inadhani kuwa mtu akiosha nyele zake anaosha elimu yote kichwani.
"Kulikuwa na kijana mmoja ambaye alikuwa haoshi nyele zake kabla ya mtihani, alikuwa msafi wakati mwingine wote ila siku ya mtihani huwezi kukaribia," amesema mwanamfunzimmoja kuhusu mwenziwe darasani.
Kula korosho
Mwezi mmoja kabla ya mitihani Hong Kong, wanafunzi hukusanyika kwa shughuli mbalimbali zinazoanza kwa chakula cha jioni kijulikanacho kama ging guo.
Inaaminika shughuli hizo husaidia wanafunzi kupita mitihani kwa alama za juu.
Ni muhimu kwa wanafunzi katika chakula hicho kula nyama ya ngurumwe kwa korosho.
Na chakulwa hicho hupatikana katika migahawa ya kichina ambapo Korosho kwa kichina ni neno sawa na neno"kutarajia kupasi ", na "nyama ya nguruwe" ni sawa na "hamu ya kupata alama ya juu".
Nguvu ya kuku
Supu ya kuku inadhaniwa kuchangamsha ubongo.
Wanafunzi wa Malaysia, Hong Kong, Singapore na China hunywa supu ya kuku wanaposoma kujitayarisha kwa mitihani na asubuhi ya kuamkia mtihani wenyewe.
"Sio uchawi," anasema Dylan Lee Soon Yoong, mwanafunzi kutoka Singapore katika chuo kikuu cha London.
"Nilikunywa supu ya kuku asubuhi kuamkia mtihani ikiwa moto moto. Inatakikana kukusaidia kuwa na makini na hunywa kwa wingi na wanafunzi Singapore."
Vaa chupi nyekundu
Rangi nyekundu inaaminika kwa ukubwa China kuwani rangi ya bahati nzuri.
Kwahivyo watu wengi wanaamini ni vizuri kuvaa nguo nyekundu na zaidi chupi ya ndani wakati wa mtihani.
Wakati mtu anapofanikiwa kuna msemo wa Kichina unaosema, "umevaa chupi nyekundu?"
Lakini Chong Wang anaonya: "baadhi ya watu huepuka kuvaa ranginyekundu wakati wa mtihani kwasababu China alama za kufeli huandikwa kwa rangi nyekundu."
KWA HABARI ZAIDI
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: