Kwa wale ambao tuna nywele asilia a.k.a natural hair,tayari tunafahamu changamoto kadhaa tunazokumbana nazo.Kwa wale mnaofikiria kuanza kuwa na nywele asilia,karibuni sana tuendelee kujuzana namna ya kutunza nywele zetu kama tulivyopewa na Mungu.
Katika mada ya leo,nitakwenda kuzungumzia vitu vya kuzingatia ili kuikuza nywele yako asilia kwa haraka zaidi.Je,unazifahamu nywele zako vizuri?Una nywele za aina gani?Zina tabia gani?Zinataka nini?
1. Kuzikubali kama zilivyo na kuzipenda.
Utasikia ..hiki kipilipili changu ni steelwire ya kimataifa, ..hakitikisiki hata upepo wa dunia yote ungevumia pande hizi.Mwingine oh..nywele zangu kama miti ya mibuyu kichwani…hazishikiki.Tatizo ni kwamba hamjafahamiana vizuri yani wewe na nywele zako.Hata mimi niligombana nazo sana huko nyuma kabla ya kuzielewa vizuri.Jenga mahusiano mazuri tu na nywele zako,zielewe,ukifikia hapo utaanza kuzipatia hata hazitakusumbua.
2. Usafi wa ngozi ya nywele na nywele zenyewe.
Nywele zenye afya huanzia kwenye ngozi safi ya nywele.Nafahamu unataka nywele zako zisidumae kwa hiyo zioshe vizuri.Wakati uliopita nilizungumzia kuziosha kwa product zilizo rafiki( ‘friendly’) .Ngozi safi ya nywele itasababisha nywele kupata njia ya kujitokeza nje kwa urahisi.Unapoziacha chafu,ule uchafu unaziba matundu ya nywele zako na kuzuia njia,kama ambavyo matundu ya uso yakiziba unapata machunusi maana uchafu unajaa basi kwa nywele hazitakua vizuri.
3. Linda unyevu wa nywele zako
Kila mtu akisikia kiu hunywa maji.Nywele zako zinahitaji kulindwa zisisikie kiu.Unapoziosha,yale mafuta asilia ya kuzilinda huondoka na uchafu.Nywele inabaki ikiwa na udhaifu fulani maana haiwezi hata kushikilia hayo maji yaliyopo vizuri,na zikikauka zinakua kavu sana.Ni vizuri kabla hazijakauka vizuri,ukazi-’condition’.Kwa nywele ambazo ni nyepesi na chache,pia kuna product za kuzisaidia ziweze kutunza vizuri unyevu na hivyo kuwa na afya nzuri.
4. Zifahamu nywele zako
Yani hapa ndo shule ilipolalia kabisaa maana ukizijua tu basi utazihudumia kwa usahihi.Unatakiwa kuangalia namna gani nywele zako zinanyonya unyevu.Unajuaje?
Chukua kikombe,kijaze maji safi.Ukipata glass itakuwa vizuri zaidi.
Chomoa unywele mmoja kichwani,hakikisha unatoka na kale kamzizi kake keupe keupe hivi.
Tumbukiza unywele wako kwenye glass yako ya maji hakikisha imeingia yote.Kama ikizama hapo hapo na hainyanyuki tena,basi nywele zako zinanyonya unyevu kwa haraka kabisa.Kama inachukua muda kuzama,au haizami kabisa,nywele zako zinanyonya unyevu taratibu au zinanyonya kwa shida.(Wala usihofu,zipo namna ya kuzifanya zinyonye unyevu kwa haraka,tutajuzana.)Ni kwamba ‘cuticle’ zake zimefunga haswa,ndio maana unyevu au maji haviingii kwa haraka.
Kwa hiyo ukifanya ‘deep conditioner’ kwa kutumia joto kama la drier lakini uwe moto mdogo sana au ufanye ‘hot oil treatment’ itakusaidia ‘cuticle’kufunguka na unyevu kupita.
Mbadala,unaweza baada ya kuosha suuza na maji ya vuguvugu halafu weka mafuta ya kimiminika.Inasaidia sana.
Mimi nina aina gani?..Nina nywele zinazonyonya unyevu haraka.
5. Mafuta ya Kupaka kichwani.
Ni ya muhimu mnoo!.Nimefanya utafiti wa kina nimeona mafuta ya nazi yanaweka afya nzuri kwa nywele aina nyingi hivyo na mimi nikaanza kuyatumia.Kwangu mimi,mafuta ya nazi ya kutengeneza mwenyewe yamenikubali sana.Japo huwa nanunua pia mafuta kama ya olive(extra virgin) na ya tea tree.
6. Kuzichambua vizuri kabla ya kuchana.
Uwe mkarimu na mwenye subira kwa nywele zako.Mimi zikijifunga huwa nazichambua kwa mikono taratibu wakati mwingine nazilowesha na maji kwa mbali halafu nachana kwa chanuo lenye mapana sio ambalo reli zake zimebanana.sio kitana.Chanuo kubwa(wide toothed comb).
7. Usizisumbue mara kwa mara na usuke mitindo ya kuzitunza zikue.
Kama unataka zikue haraka,usizisumbue sana.Unaweza ukasuka mitindo mizuri tu ukakaa nazo wiki nzima au kadri zitakavyodumu.Au upunguze kuzichana mara kwa mara lakini utafute siku kama wikiendi ukae uzichambue taratibu na vidole kuondoa mafundo.Kuchana mara kwa mara zinapukutika,zinaanguka.Zitakua lakini sio kwa kasi ya kama ukizisuka ukaziacha kwa muda.
8. Punguza matumizi ya vitu vya moto kwenye nywele zako kama pasi ya nywele na vingine vya hivyo.
Mimi dryer la nywele situmii zaidi ya mara mbili kwa mwezi.Mara nyingi naziacha zikauke na hewa hata kama nimezifunga rollers natoa kesho baada ya masaa 24.
KWA HABARI ZAIDI
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
Ahsante sana kwa darasa zuri naomba msaada: Nywele zangu hukua vizuri sana lakini zikishakuwa ndefu huakatika na kunifanya hata niweke madawa japo siyapendi. Sasa ivi Nina mwaka nimeacha kuweka dawa, zile za dawa zote zimekatika zimeanza natural na ninapenda kubaki natural nisaidie nifanyeje zisikatike
ReplyDeleteHello,
ReplyDeleteHii ni kuwajulisha kwa ujumla kwamba Mheshimiwa John Kerry Jemmy, mkopeshaji binafsi, ana fursa ya kifedha kwa mtu yeyote anayehitaji msaada wa kifedha kwa wanafunzi, mikopo ya kibiashara, mikopo ya uwekezaji, uimarishaji wa madeni na mengi zaidi. Umekataliwa na mabenki na mashirika mengine ya kifedha? Usione tena, kwa sababu tuko hapa kwa matatizo yako yote ya kifedha, tunatoa mikopo kwa kiwango cha 2% kwa watu binafsi na makampuni katika hali wazi na inayoeleweka. Hakuna kuangalia hundi ya mikopo, 100% ya uhakika. Wasiliana nasi leo na utakuwa na furaha kufanya hivyo kwa sababu tuko hapa kutimiza tatizo lako lote na historia ya kifedha.
Tutumie barua pepe kwa: (creditcashexpress8@gmail.com)