sponsor

Slider

T - SHIRT PRINTING


LARGER FORMATING

STICKERS BRANDING | LARGE FORMATING


MIFUKO PRINTING

SMALL FORMATING

WEDDING | KITCHEN PART | SEND OFF | INVITATION CARDS

POSTERS | CARTOON | PHOTO PRINTING

» » » TUUNGE MKONO HAKI SAWA NA USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA MAENDELEO.

02

Watanzania na wadau wa haki za wanawake nchini wameshauriwa kuunga mkono haki sawa na ushiriki kwa wanawake katika fursa za uongozi wa kisiasa na kiuchumi na kupima mafanikio yaliyofikiwa na kuweka mipango yenye matokeo makubwa. 
 
Akitoa taarifa juu ya siku ya wanawake Duniani, Katibu Mkuu Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Wanawake Bi Sihaba Nkinga amesema kuwa siku ya wanawake Duniani husisitiza kujenga mshikamano wa wanawake wote duniani, kuhamasisha jamii kutafakari kauli mbiu ya Maadhimisho ya siku  hiyo ya kila mwaka.
 
Amesisitiza kuwa wananchi wametakiwa  pia  kubainisha shuhuda za wanawake waliotoa mchango uliotukuka katika kuwezesha maendeleo ya wanawake na taifa kwa ujumla na Tafakuri hii hufanywa kwa kuelimisha jamii kuhusu jitihada mbalimbali zilizofanywa na Serikali na asasi mbalimbali yakiwemo Mashirika yasiyo ya Kiserikali katika kuwaendeleza wanawake na kuhamasisha jamii kuhusu utekelezaji wa sera na mipango mbalimbali ya Serikali yenye lengo la kudumisha Amani, Usawa na Maendeleo kwa wanawake kwa ujumla.
 
“Kuanzia mwaka 2005 Serikali ilipitisha uamuzi kuwa, maadhimisho haya yafanyike Kitaifa kila baada ya miaka mitano ili kutoa muda wa utekelezaji wa maazimio na kupima mafanikio yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka mitano”Alisema Bi Sihaba.
 
Sihaba Nkinga amewashauri wanahabari wote kuelimisha jamii kuhusu kauli mbiu ya Siku ya Wanawake kwa mwaka 2016 inayosema “50 – 50 Ifikapo 2030; Tuongeze Jitihada”ambapo Kauli mbiu hii inasisitiza kuwa na mikakati thabiti yenye mwelekeo wa kufikia Agenda ya 2030 yenye malengo ya kufikia asilimia 50 kwa 50 ya ushiriki wa wanawake na wasichana katika nyanja zote za maendeleo.
Aidha Bi Sihaba Nkinga amemtaka kila Mtanzania aweze kutambua jukumu alilonalo katika kufikia lengo la ushiriki sawa wa wanawake na wasichana katika Uchumi; Afya, Elimu, Ajira, Sheria na Siasa ifikapo mwaka 2030.
 
Kwa mwaka  2016, katika kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani,mikoa yote nchini itazingatia hali na mazingira ya mikoa husika na kwa  mkoa wa Dar es Salaam siku hii itaadhimishwa  katika Manispaa ya Kinondoni. Wizara inatoa wito kwa mikoa yote kuhamasisha wananchi na wadau wote kushiriki maadhimisho ya siku hii adhimu na kuzingatia ujumbe wa kauli mbiu ya mwaka 2016.

Asante sana kwa kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea website hii
Pia waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini

INSTAGRAM           FACEBOOK    GOOGLE +    PINTEREST   TWITTER       

LINKEDIN     DRIBBBLE    NOTJUSTOK



Karibu sana
LINK CLASSIC

BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI

CODE HAPA

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply