Zikiwa zimepita siku tano tangu Rais John Magufuli aeleze kushangazwa na vitendo vya askari wa polisi kunyang’anywa bunduki na majambazi, polisi mkoa wa Dodoma wameporwa SMG.
Watu saba wanaosadikiwa kuwa majambazi walifanya uporaji huo baada ya kuvamia ofisi za kampuni ya simu za mikononi ya Halotel katika eneo la Medelii, Manispaa ya Dodoma, na kuwajeruhi askari polisi waliokuwa zamu.
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa hapa, David Mnyambuga, tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana, saa nane na nusu usiku katika ofisi hizo.
Alisema watu hao wakiwa na mapanga na nondo, walivamia ofisi hizo na kutoboa ukuta na kisha kuwajeruhi askari polisi kwa mapanga na kupora SMG hiyo.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa alisema jeshi hilo linamshikilia mtu mmoja ambaye anaendelea kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo, na kwamba msako mkali bado unafanyika ili wahusika wote waweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.
LINK
CLASSIC: Asante sana kwa kutembelea Website hii coz ni moja
ya Support kwetu mungu akubariki sana pia endelea kusoma na kufungua LEBAL
zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya Website hii bila kusahau
kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea website hii
Pia waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
Karibu sana
LINK CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA


No comments: