KALENDA za zamani ziliutumia mwezi wa angani ziliitwa “Lunar Calender”, Tarehe 1 ya mwezi ilikuwa siku ulipoandama yaani
Mwezi-Mdogo (Crescent Moon). Mwezi unapofika siku ya 14unakuwa
umefikia ukubwa wa juu na huitwa “Mwezi-Mkubwa au Full Moon”.
Mwaka 45KK, Julius Caesar alitangaza kalenda mpya mpya ikaitwa “Julian
Calendar” yenye siku 365 ikijulikana kwamba jua huzunguka dunia kwa
siku 365.25.
Hivyo pengo la Kalenda na mzunguko likabaki robo siku, Robo hiyo
itafidiwa kila baaada ya miaka minne mwishoni mwa mwezi February,
Inapofidiwa hivyo huitwa mwaka-mrefu (Leap year) kwa sababu una siku
366.
Mwaka mrefu ukachaguliwa kuwa ni ule unao gawanywa kwa nne mfano 1700,1800, 1900, 2100,2300. Baadaye iligundulika kuwa, kumbe Jua huzunguka kwa siku 365.24218967 ziitwazo “Tropical Year”. Hizi ni chache kuliko siku nzima 365.25 zilizokadiriwa mwanzoni.
Uchache huu husababisha
kuwe na pengo la dakika 11 na sekunde 14.812512 kwa mwaka.
Pengo hili ni dogo, lakini hupanuka hadi kuwa siku nzima kila baada ya
miaka 128.0355 Mwaka 1545 lilivuka siku 9.25.
Kuondoa tatizo hili Papa Gregory XIII aliamuru iundwe kalenda mpya na
akachagua oktoba 4,1582 iwe siku ya mwisho kutumika “Julian Calendar”
.Kesho yake, Kalenda mpya ikaanza kutumika unge tarajia hiyo kesho iwe
ni oktoba 05, 1582.
Lakini ili uzibe pengo lile lililofikia siku kumi, ilibidi kalenda
mpya kuziruka siku hizo kumi. Hivyo hii mpya iliyoitwa “Gregorean
Calendar” ikaanza kama Oktoba 15 badala ya Oktoba 05. Watu walilala
oktoba 04, 1582 kesho yake wakaamka ikiwa ni Oktoba 15, 1582.

Pasaka imetajwa kwenye Biblia hivi: ” Mwezi wa kwanza, siku ya kumi na
nne ya mwezi, wakati wa jioni ni Pasaka ya BWANA , na siku ya 15 ya
mwezi huo ni sikukuu ya BWANA, ndiyo siku ya mikate isiyotiwa
chachu (Walawi 23:5)…”. Hivyo pasaka ni tarehe ya 15 ya mwezi wa
kwanza.
Lakini Biblia pia inautaja mwezi wa kwanza kwa jina la Nisan (Esta3:7,Nehemia 2:1).
Yesu alisulubiwa mwaka ambao Ijumaa iliitangulia pasaka kwa siku moja
(Yohana 18:28, Marko 15:42-43). Hivyo tarehe ya yesu kusulubiwa ni
Ijumaa, Nisan 14, yaani siku moja kabla ya Nisani 15 au siku mojakabla
ya Mwezi Mkubwa.
Baadaya ya Yesu, wakristo waliiadhimisha Pasaka siku ya ufufuko yaani
Jumapili, lakini walibishana iwe ni Jumapili ipi?.
Mwaka 325 Kanisa Katoliki liliamua kuondoa ubishi huo lilipokutana
Nicaea, likaweka kanuni maalumu ya kuipata pasaka kama ifuatavyo.
Hatua ya kwanza ni kutambua tarehe ya “Equinox”, ambayo ni Machi 21,
ambako ndiko kwenye mwezi wa kwanza wa kibiblia ambao tumeona unaitwa “Nisan”.
Hatua ya pili ni kupata tarehe ya “Mwezi-Mkubwa” utakaoonekana baadaya
hii “Equinox”. Hatua ya tatu ni kuipata Pasaka ambayo Jumapili baada ya
huu “Mwezi-Mkubwa”.
Kwa sababu mwezi huzunguka kwa siku 29, basi mwezi “Nisan” ambao una
Pasaka, ni ule uliomo ndani ya siku ya 29 kuanzia siku ya “Equinox”,
yaani machi 21 hadi Aprili 18.
Hivyo hata Pasaka ya Mwaka huu inatarajiwa kusherekewa tarehe 27 machi 2016 siku ya Jumapili ambapo Mtembezi Media Group inakutakia mapumziko mema ya Sikukuu ya Pasaka (Kufufuka kwa Bwana).
LINK
CLASSIC: Asante sana kwa kutembelea Website hii coz ni moja
ya Support kwetu mungu akubariki sana pia endelea kusoma na kufungua LEBAL
zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya Website hii bila kusahau
kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea website hii
Pia waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
Karibu sana
LINK CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA



No comments: