KAIMU Kocha Mkuu wa Simba, Mrundi, Masoud Djuma ametamka kuwa mshambuliaji wake Mganda, Emmanuel Okwi anatarajiwa kuwepo kwenye orodha ya wachezaji atakaowatumia kesho mechi dhidi ya Singida United.
Hiyo, ikiwa ni siku moja tangu mshambuliaji huyo ajiunge na timu hiyo kwenye kambi ya pamoja ya maandalizi ya mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Singida itakayochezwa kesho Alhamisi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Okwi amejiunga na kambi hiyo akitokea nyumbani kwao Uganda alipokwenda baada ya kuwa majeruhi.
Akizungumza na Championi Jumatano, Djuma alisema mshambuliaji huyo amerejea akiwa bado yupo fiti ambaye leo (jana), asubuhi alifanya mazoezi ya nguvu ya pamoja na wenzake kwa ajili ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Singida. Djuma alisema, mshambuliaji huyo amefanya mazoezi vizuri kwa kufanya programu zote za kukimbia mbio fupi na ndefu kabla ya kuchezea mpira.
Aliongeza kuwa, Okwi kesho (leo) asubuhi atafanya mazoezi ya mwisho ya pamoja na wenzake kabla ya mchana kurejea jijini Dar es Salaam wakitokea Morogoro walipokwenda kuweka kambi ya kujiandaa na mechi dhidi ya Singida.
“Okwi alirejea Dar jana (Jumatatu) na siku hiyo jioni alifika hapa mkoani Morogoro ambako tumeweka kambi kwa ajili ya mechi dhidi ya Singida tutakayocheza kesho (Alhamisi). “Mara baada ya kufika leo (jana) alifanya mazoezi ya pamoja na wenzake kabla ya kesho (leo)
Jumatano asubuhi kufanya mazoezi ya mwisho kabla ya timu kurejea Dar kwa ajili ya mechi dhidi ya Singida ambayo yeye anatarajiwa kuwepo kwenye orodha ya wachezaji nitakaowatumia, hakika naamini kuwa huyu ni mchezaji muhimu na ataisaidia sana timu hii,” alisema Djuma.
KWA HABARI ZAIDI
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: