sponsor

Slider

T - SHIRT PRINTING


LARGER FORMATING

STICKERS BRANDING | LARGE FORMATING


MIFUKO PRINTING

SMALL FORMATING

WEDDING | KITCHEN PART | SEND OFF | INVITATION CARDS

POSTERS | CARTOON | PHOTO PRINTING

» » » KWA SIMBA HII, MNAPIGWA KAMA MLIVYOKUJA

Kikosi cha timu ya Simba.
MAKOCHA wa Simba wameweka mikakati kabambe ya kuhakikisha wanatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara na kufanya vizuri katika Kombe la Shirikisho Afrika mwezi ujao. Kocha Msaidizi wa Simba, Mrundi, Masoud Djuma, amesema ujio wa Kocha Mkuu Mfaransa, Pierre Lechantre, utachangia timu yao kutwaa taji hilo la ligi kuu na kufanya vizuri kimataifa mwaka huu.

Djuma ametoa kauli hiyo ikiwa kesho Jumapili timu yake ikitarajiwa kucheza na Majimaji ya Songea mechi ya ligi kuu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kocha huyo ametamka hayo ikiwa ni siku mbili zimepita tangu aanze kufanya kazi pamoja na Lechantre katika kukinoa kikosi cha Simba kinachoongoza ligi kuu kikiwa na pointi 32. Mfaransa huyo, alitua nchini wiki iliyopita na kusaini mkataba wa miezi sita pamoja na msaidizi wake mwingine raia wa Tunisia, Mohammed Aimen na tayari wameanza kazi pamoja.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Djuma alisema ndani ya wakati wanataka kuona timu yao ikifanya vizuri katika ligi na michuano ya kimataifa ili kufanikisha malengo yao.


Djuma alisema kwa kushirikiana na kocha huyo Mfaransa, wanaendelea kukiboresha kikosi chao kuanzia safu ya ulinzi, kiungo na ushambuliaji ili kuhakikisha makosa hayajirudii. “Kila siku kabla na baada ya mazoezi huwa tunafanya kikao na wachezaji na kikubwa tunawasisitizia malengo yetu ya kuchukua ubingwa wa ligi na kufika mbali kwenye michuano ya kimataifa.

“Tunataka kuona kila mchezaji anacheza kwa kujituma na kutimiza wajibu wake kama unavyoona ushindani umeongezeka kwa kiasi kikubwa,” alisema.

Akizungumzia mchezo dhidi ya Simba, Kocha wa Majimaji, Peter Mhina, alisema yeye amebaki Songea lakini msaidizi wake Habib Kondo jana mchana alisema; “Bado tupo njiani kwenda Dar es Salaam, lakini tutapambana kushinda mechi hii.”

KWA HABARI ZAIDI

BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI

CODE HAPA

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply