DAKTARI wa Yanga, Edward Bavu amesena kuwa majeraha ya mara kwa mara yanayomkabili straika wa timu hiyo, Amissi Tambwe, yanatokana na aina ya uwanja ambao wamekuwa wakifanyia mazoezi kuwa mgumu na usio rafiki kwa wachezaji kufanya mazoezi.
Tangu kuanza kwa msimu huu amekuwa nje ya kikosi hicho kutokana na majeraha ya goti kujirudiarudia ambayo yamemfanya kwenye mechi 15 za timu hiyo kucheza mara tatu tu na kukosa mechi 12. Mechi zote hizo hajafunga hata bao moja.
Akizungumza na Spoti Xtra, Bavu amesema kuwa Uwanja wa Uhuru ambao ndiyo wanafanyia mazoezi una eneo gumu la kuchezea ambapo ili ucheze unahitaji kuvaa viatu maalum na siyo vyenye meno.
“Unajua kwa sasa tunakabiliwa na majeruhi wa kila mara kama ilivyo kwa Tambwe na wengine kwa sababu ya hapa tunapofanya mazoezi kuwa na eneo gumu la kuchezea pichí na lisilo rafiki kwa wachezaji kucheza.
“Hasa wachezaji wanapocheza na viatu vyenye meno ndiyo wanazidi kujiumiza na unaona kila mara kuna kundi la majeruhi, ili kuepuka jambo hilo inabidi wachezaji wote wawe na viatu maalum ambavyo havina meno ili waweze kucheza kwa raha bila ya hivyo majeruhi watakuwa hawakosekani,” alisema Bavu
KWA HABARI ZAIDI
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: