Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe amekagua mradi mkubwa wa maji wa Ziwa Victoria katika jimbo la Nzega Mjini.
Mradi huo ni moja kati ya miradi mikubwa ya maji nchini huku ukitarajiwa kutumia zaidi ya Bilioni 600 ambazo zilitiliwa saini baina ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya India mwezi May, 2017.
Bashe amesema “tayari mkandarasi ameanza ujenzi wa matanki makubwa ya maji na njia za kupitisha mabomba makubwa ambayo yataifanya Nzega Mjini kuwa kitovu kikuu cha usambazaji wa Maji haya ya Ziwa Victoria:.
Katika kuhakikisha mradi huo unanufaisha wananchi wote wa Jimbo la Nzega Mjini Bashe aliwasilisha maombi binafsi kwa Rais Dr. John Magufuli ya fedha kwa ajili ya kupanua mtandao wa Maji Nzega na tayari Rais amekwisha kutoa fedha hizo ili kuboresha upatikanaji wa Maji ya uhakika katika Mji wa Nzega.
Bashe pia ametembelea eneo la Sagara ambapo kwa kushirikiana na Halmashauri ya Mji wa Nzega wamekusudia kujenga kisima kikubwa chenye uwezo wa kusambaza maji kwenye maeneo jirani. Upanuzi wa kisima hicho ni katika juhudi mahsusi za kuhakikisha hakuna tena tatizo la maji Nzega.
Kuhusiana na ajira zitakazotokana na mradi huo Bashe amesema “Kipaumbele kwa ajira ambazo zitatokana na mradi huu watapewa watanzania ambao wanaoishi katika maeneo ambayo mradi unapita ili kuhakikisha mzunguko wa fedha na ajira zinakuwepo kwa vijana na wananchi ndani ya Mji wa Nzega”.
KWA HABARI ZAIDI
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: