sponsor

Slider

T - SHIRT PRINTING


LARGER FORMATING

STICKERS BRANDING | LARGE FORMATING


MIFUKO PRINTING

SMALL FORMATING

WEDDING | KITCHEN PART | SEND OFF | INVITATION CARDS

POSTERS | CARTOON | PHOTO PRINTING

» » » MGHANA MPYA AWASILI RASMI AZAM FC


MSHAMBULIAJI mpya wa Azam FC, Bernard Arthur, amewasili asubuhi ya leo Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam tayari kuanza maisha mapya Chamazi.

Arther aliyesaini miaka miwili na klabu hiyo akitokea kwenye timu ya Liberty Professional ya kwao, Ghana, amewasili leo akiongozana na Mtendaji Mkuu wa Azam, Abdul Mohamed ambaye alimfuata nchini humo kukamilisha usajili wake.

Akizumgumza mjini Dar es Salaam leo, Ofisa Habari wa Azam, Jafari Idd alisema kuwa, mchezaji huyo tayari ameungana na timu huku akisubiri uongozi wa klabu hiyo wakishughulikia vibali yake kwa ajili ya kuanza kazi rasmi.

“Mchezaji wetu mpya wa Ghana, amewasili alfajiri ya leo nchini akiwa na Mtendaji mkuu wa Azam, Abdul Mohamed, tayari ameungana na timu Chamazi huku akisubiri uongozi kushughulikia vibali vyake ili aweze kuanza kazi rasmi,” alisema Jafari.

Usajili wa Arthur ni sehemu ya mapendekezo ya benchi la ufundi la timu hiyo kwenye usajili huu wa dirisha dogo, anayekuja kuziba pengo la straika mwingine, Yahaya Mohammed, aliyeondoka kwa makubaliano maalumu ya pande mbili wiki chache zilizopita.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa timu ya WAFA (Ghana) na Asec Mimosa ya Ivory Coast, anaungana na washambuliaji wengine wa timu hiyo katika kukiongezea makali kikosi hicho, ambao ni Mbaraka Yusuph, Wazir Junior, Yahya Zayd, Shaaban Idd pamoja na wale waliopandishwa kutoka Azam B, Paul Peter na Andrea Simchimba.

Wakati huo huo Jafari alisema timu inajiandaa kwa ajili ya mechi yao ya kesho dhidi ya Mtibwa Sugar a Morogoro, mchezo wa raundi ya 11 ya Ligi Kuu Bara utakaopigwa kuanzia saa moja usiku kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Katika hatua nyingine, nyota wawili wa Azam FC, Shaaban Idd na Joseph Kimwaga, waliokuwa majeruhi sasa huenda wakarejea dimbani Januari Mosi mwakani wakati timu hiyo ikishiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar.

Mbali na kufanya programu ya mazoezi ya gym, Idd tayari ameruhusiwa kuanza mazoezi madogo madogo ya kucheza na mpira na kukimbia mwanzoni mwa wiki hii huku Kimwaga akiendelea na mazoezi ya gym aliyoanza mwezi mmoja uliopita.

Daktari wa Azam FC, Mwanandi Mwankemwa, amesema kwamba wachezaji hao wapo kwenye kipindi cha mwisho cha tiba yao cha kuwarejesha katika hali yao ya kawaida huku akidokeza Idd ataendelea na programu hiyo na anatarajiwa kurejea dimbani kuanzia Januari Mosi.

“Kimwaga kidogo kumetokea matatizo kidogo katika ukunjaji wa goti lake baada ya operesheni kwa hiyo sasa hivi bado anafanya mazoezi ya kukunja goti na pindi atakapokuwa ameweza kukunja goti vizuri naye ataruhusiwa kuanza kucheza mpira kidogo kidogo na kukimbia naye pia tutamtarajia itakapofika Januari Mosi atarudi tena kiwanjani kwenye ushindani,” alisema.

Idd anasumbuliwa na majeraha ya nyonga yake ya mguu wa kulia huku Kimwaga akisumbuliwa na goti la mguu wa kushoto kwa pamoja walifanyiwa upasuaji nchini Afrika Kusini na tokea waanze mazoezi ya gym wamekuwa chini ya uangalizi wa daktari wa Azam FC na wataalamu wa Kliniki ya London Health Centre, iliyopo eneo la Macho, Msasani jijini Dar es Salaam wanakofanya mazoezi ya gym.



KWA HABARI ZAIDI

BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI

CODE HAPA

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply