sponsor

Slider

T - SHIRT PRINTING


LARGER FORMATING

STICKERS BRANDING | LARGE FORMATING


MIFUKO PRINTING

SMALL FORMATING

WEDDING | KITCHEN PART | SEND OFF | INVITATION CARDS

POSTERS | CARTOON | PHOTO PRINTING

» » » KERO YA UMEME KANDA YA KUSINI YAPEWA AGIZO



Mkuu wa mkoa wa lindi Godfrey Zambi ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania Tanesco kanda ya kusini, kuhakikisha kuwa umeme unaozalishwa na kituo cha umeme kinachotumia gesi asilia mkoani Mtwara kugawa umeme sawa katika mikoa ya lindi na mtwara, ili kuondoa kero ya kukatika mara kwa mara kwa umeme mkoani lindi.

Zambi amesema hayo mkoani mtwara alipofanya ziara ya siku moja kutembelea kituo cha uzalishaji umeme kinachotumia gesi asilia ili kuona hali halisi ya uzalishaji umeme katika kituo hicho na changamoto zilizopo.

Mkuu wa mkoa wa lindi Godfrey Zambi amelitaka shirika la umeme Tanzania Tanesco kanda ya kusini kuangalia upya kiwango kikubwa cha kukatika katika kwa umeme mkoani lindi na kutaka umeme unaozalishwa katika kituo hicho cha mtwara unatumika sawa katika mikoa hiyo ya lindi na mtwara bila ya kuwepo tofauti huku akiishukuru serikali kwa jitihada za kuhakikisha kuwa umeme unarejea katika hali yake ya kawaida siku chache zijazo.

Kwa upande wake Meneja wa kituo cha kuzalisha umeme mkoani mtwara Mhandisi Mkulungwa Chinumba amesema Tanesco inaendelea na kazi ya matengenezo ya mitambo ya kuzalisha umeme na itahakikisha mitambo yote inatengenezwa ili irejehe katika hali yake ya kawaida ya uzalishaji wa umeme .

Katika ziara yake hiyo ya siku moja Mkoani Mtwara mkuu wa mkoa wa lindi Godfrey Zambi pia ametembelea bandari ya mtwara kuona jinsi kazi ya usafirishaji wa korosho unavyoendelea na maendeleo ya upanuzi wa bandari hiyo na kutoa wito kwa wanunuzi wa zao la korosho kutumia bandari hiyo kusafirisha korosho zao.

BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI

CODE HAPA

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply