sponsor

Slider

T - SHIRT PRINTING


LARGER FORMATING

STICKERS BRANDING | LARGE FORMATING


MIFUKO PRINTING

SMALL FORMATING

WEDDING | KITCHEN PART | SEND OFF | INVITATION CARDS

POSTERS | CARTOON | PHOTO PRINTING

» » » DALILI ZIFUATAZO ZINAONYESHA KAMA UNAUPUNGUFU WA MAJI MWILINI

 DALILI ZIFUATAZO ZITAONYESHA UNAUPUNGUFU KAMA UNAUPUNGUFU WA MAJI MWILINI

UNGANA NA
LINK CLASSIC
KILA SIKU KWA HABARI MPYA



Umeshawahi kwenda hospitali kumlalamikia daktari kuwa mwili wako hauna nguvu na unajisikia kuchokachoka sana na baada ya kukuchunguza, akakwambia huna tatizo lolote isipokuwa una upungufu wa maji mwilini tu?

Mwili kuishiwa nguvu huwa ni miongoni mwa dalili za upungufu wa maji mwilini na chanzo kikiwa ni wewe mwenyewe kutopenda kunywa maji. Ni kawaida kwa baadhi ya watu kutokunywa maji hadi pale wanaposikia kiu.

Katika makala ya leo, nitakujuza dalili za mwili kuishiwa maji ambazo hujitokeza na kukuhimiza kunywa maji hata kabla hujasikia kiu. Uonapo dalili hizo, hupaswi kuzipuuzia bali kunywa maji kwa wingi tena haraka.

Upungufu wa maji mwilini ni nini?

Pale mwili unapopoteza kiasi kingi cha maji kwa njia mbalimbali, ikiwemo jasho na mkojo, mwili hupungukiwa maji na hivyo mtu huyo huambiwa ana upungufu wa maji. Tunaelezwa kuwa karibu theluthi mbili ya miili yetu imejaa maji.

Ili mwili uweze kufanya kazi yake vizuri, kiwango cha maji mwilini hakipaswi kupungua hata kidogo, hivyo kila mtu ana wajibu wa kunywa maji ya kutosha kila siku ili kulinda kiwago chake cha maji kisipungue na kinapopungua ndipo hapo mwili huanza kuonesha dalili za kukaukiwa maji (dehydration).

Nini chanzo cha upungufu wa maji mwilini?

Sababu zinazosabababisha mwili kukaukiwa maji huweza kuwa nyingi, lakini zinazojulikana zaidi ni pamoja na:

1. Kuacha kunywa maji

2. Kukaa kwenye joto kwa muda mrefu

3. Kunywa kiwango kikubwa cha pombe,

4. Ungonjwa wa kisukari ambao husababisha mtu kukojoa mara kwa mara

5. Kutokwa na jasho jingi, kwa sababu ya ama kufanya kazi ngumu au mazoezi. 

Hivyo inashauriwa mtu anayetokwa jasho jingi kunywa maji mara kwa mara wakati akiendelea na shughuli inayomtoa jasho.

6. Kama ukiugua au ukipatwa na homa kali, huweza kupungukiwa na maji mwilini

7. Kutapika na kuharisha nako huweza kupoteza maji mwilini.

Dalili za kupungukiwa maji kwa watoto

Kwa kawaida, dalili za upungufu wa maji mwilini hujitokeza zaidi kwa watoto wadogo kuliko watu wazima au wazee. Dalili za upungufu wa maji mwilini kwa watoto huweza kusabababishwa ama na kuharisha, kutapika, kutokunywa maji au vimiminika vingine vya kutosha.

Mtoto mwenye dalili za upungufu wa maji huweza kuonesha dalili zifutazo:

1. Kukojoa mara chache sana

2. Mtoto kutokuwa mchangamfu

3. Macho, tumbo au mashavu kubonyea

4. Mdomo na ulimi kukauka

5. Mtoto kulia mara kwa mara na anapolia machozi hayatoki.

Dalili za kupungukiwa maji kwa wazee

Dalili za upungufu wa maji kwa wazee ni tofauti na watu wazima. Wazee wa umri zaidi ya miaka 60 huwa na ngozi iliyosinyaa na hata ukiiminya, hubaki katika hali hiyo kwa muda na unapoikwaruza alama hubaki.

Halikadhalika, wazee hukosa haja ndogo kwa muda mrefu, hupungukiwa uzito kwa kiasi kikubwa na hupatwa na homa.

Dalili za kupungukiwa maji kwa wajawazito

Upungufu wa maji mwilini kwa waja wazito ni hatari kwa mama pamoja na mtoto. 

Dalili zinazoweza kujitokeza kwa waja wazito ni pamoja na:

1. Kukojoa mkojo wa njano nyeusi

2. Kuumwa na kichwa

3. Mwili kukosa nguvu

4. Kichefuchefu na kutapika

5. Kukaukwa na mdomo

Ili kujiepusha na matatizo ya upungufu wa maji na hatimaye kujikuta unakumbwa na dalili kadhaa zilizoelezewa hapo, ambazo ziko pia kwa watu wazima wengine, ni kuwa na mazoea ya kunywa maji ya kutosha kila siku.

Hata utakapozidiwa na kukimbizwa hospitali, hakuna dawa nyingine utakayopewa zaidi ya maji (re-hydrating solution). 

Kwa nini usubiri hali hiyo ikutokee wakati unaweza kuizuia kwa kunywa maji tu



Asante sana kwa kutembelea Website hii Mungu akubariki sana

+255 (0) 652989873 – Whatsapp / Call

Karibuni sana
LINK CLASSIC

LIKE PAGE ZETU 



"KWA HABARI ZAIDI "

BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI

CODE HAPA

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply