UNGANA
NA
LINK CLASSIC
KILA
SIKU KWA HABARI MPYA
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa siku saba kwa Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Idd Kimanta kumaliza mgogoro wa Ardhi wa Kijiji cha Emairete kilichopo Monduli Juu mkoani Arusha ambao umedumu kwa miaka 20.
Mgogoro huo ni wa shamba kubwa ambalo linamilikiwa na Kampuni ya Bia Tanzania ambalo baadaye shamba lilirudishwa kijijini, lakini viongozi wa zamani wa kijiji hicho walijimilikisha kinyemela.
Waziri Mkuu alitoa agizo hilo baada ya kusimamishwa njiani katika kijiji hicho na wananchi waliokuwa wamebeba mabango ya kumuomba msaada wa kutatuliwa mgogoro huo akiwa anatoka nyumbani kwa Edward Moringe Sokoine alipokwenda kuwasalimia wajane wa Sokoine pamoja na kuweka shada la maua katika kaburi hilo.
Waziri Mkuu alimtaka Mkuu wa Wilaya kutoa majibu ya kwa nini uongozi wa wilaya umeshindwa kutekeleza maagizo ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ambaye alifika kijijini hapo na kutoa maelekezo.
Akijibu hoja hiyo, Kimanta alikiri kuwepo kwa mgogoro huo kwa miaka 20 na kwamba Waziri Lukuvi alitoa maelekezo ambayo halmashauri inayafanyia kazi na kwamba imeshindwa kuleta majibu kwa wananchi hao kutokana na ziara ya Waziri Mkuu.
Kutokana na hali hiyo, Waziri Mkuu alitoa siku saba kwa mkuu huyo wa wilaya kuhakikisha wanashughulikia mgogoro huo kwa kutekeleza maagizo ya waziri wa ardhi.
“Natoa siku saba kuanzia leo uhakikishe mnatekeleza maagizo ya Waziri wa Ardhi juu ya mgogoro huu ili wananchi waweze kupata haki yao ya msingi,” alieleza Majaliwa.
Baada ya maelekezo hayo, aliwataka wananchi hao kuendelea kuwa na imani ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais John Magufuli ambayo ipo kwa ajili ya kusaidia wananchi wanyonge.
Awali akizungumza na wajane wawili pamoja na watoto wa marehemu Sokoine alikokwenda kuwajulia hali, Waziri Mkuu Majaliwa alisema serikali itaendelea kuenzi mema yote yaliyofanywa na Waziri Mkuu huyo aliyefariki kwa ajali ya gari mkoani Morogoro, Aprili 12, 1984.
Alisisitiza kuwa serikali inatambua kazi nzuri na mchango mkubwa wa Sokoine katika taifa na itaendelea kuenzi na kushirikiana na familia katika mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutoa huduma ya afya. vijiji 120 vya maeneo husika.
Asante sana kwa kutembelea
Website hii Mungu akubariki sana
Karibuni sana
LINK CLASSIC
LIKE PAGE ZETU
"KWA
HABARI ZAIDI"
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: