Machinjio ya Vingunguti yaliyofungwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa Nchini (TFDA) kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa kutokana na uchafu uliokithiri pamoja na kuhatarisha afya za walaji nyama , yanatarajiwa kufunguliwa siku ya Jumatatu baada ya kufanyika ukarabati mkubwa na uwekaji wa miundombinu na maji uliogharimu kiasi cha Shilingi milioni 85.
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Saidi Kumbilamoto pamoja na Maafisa Afya na Mifugo wametembelea na kukagua machinjio hayo na kujionea uboreshwaji mkubwa wa miundombinu ya kupitishia maji, ujenzi wa makaro mapya, uwekaji wa mabomba ya maji pamoja na hokey mpya kwa ajili ya kuchinjia ng’ombe.
UNGANA NA
LINK CLASSIC
KILA SIKU
Akizungumza mara baada ya ukaguzi huo , amesema tayari Ofisi ya Manispaa imefuatilia TDFA ambapo wanatarajia kupeleka barua rasmi ya kukamilika kwa ukarabati huo ambao kwa kiasi kikubwa umesababisha upungufu wa nyama pamoja na kupanda kwa bei ya nyama katika Jiji la Dar es Salaam.
Baadhi ya wachinjaji pamoja na wafanyabishara wa nyama wamepongeza ukarabati huo licha ya kulalamikia ukosefu wa kazi katika kipindi cha mwezi mmoja ambacho ukarabati wa machinjio hayo ukifanyika.
Nje ya machinjio hayo biashara ya nyama ilikuwa ikiendelea kufanyika ingawa usalama wake ulikuwa wa mashaka kutokana kutokuwa na uhakika wakujua wamechinjwa eneo gani au wamethibishwa na kitengo cha afya kama inavyofanyika ndani ya machinjio.
LINK CLASSIC: Asante sana kwa
kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia
endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya
Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea
website hii
Pia
waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
+255
(0) 652989873 whatsapp
Karibu sana
LINK CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: