sponsor

Slider

T - SHIRT PRINTING


LARGER FORMATING

STICKERS BRANDING | LARGE FORMATING


MIFUKO PRINTING

SMALL FORMATING

WEDDING | KITCHEN PART | SEND OFF | INVITATION CARDS

POSTERS | CARTOON | PHOTO PRINTING

» » » AUAWA AKITOROKA KUONESHA SILAHA KWA MGANGA WA KIENYEJI

UNGANA NA
LINK CLASSIC
KILA SIKU KWA HABARI MPYA

MTUHUMIWA wa ujambazi Amos Haruna maarufu kama George, amekufa akikimbizwa hospitalini baada ya kulipuliwa na risasi wakati akijaribu kuwatoroka polisi.

Mtuhumiwa huyo ambaye alikamatwa katika harakati za kufanya ujambazi eneo la Ulowa, Kahama mkoani Shinyanga akiwa na bunduki aina ya SMG alipohojiwa alisema kwamba ana bunduki nyingine ambayo ipo kwa mganga wa kienyeji na kukubali kuwapeleka polisi kwa mganga huyo.

Lakini walipofika eneo la Busoka, mtuhumiwa huyo alijaribu kuwatoroka askari ndipo walipompiga risasi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Muliro Jumanne alisema tukio linalomhusu Haruna (George) mkazi wa Mhungula, lilitokea juzi saa saba mchana akiwa na SMG K 5380 na gari namba T 794 BZP Toyota Crester.

Pia alikuwa na shuka la kimasai na koti na risasi 30 zilizokuwa katika kasha moja pamoja na risasi nyingine nane.

Kamanda Muliro alisema safari ya kwenda kwa mganga wa kienyeji ilitokana na mtuhumiwa huyo kukiri kuhusika na matukio ya ujambazi katika maeneo ya Bijampola, Mwakitolyo, Mbogwe, Ushirombo, pamoja na Geita na kusema bunduki nyingine ipo kwa mganga.

Kamanda alisema Haruna alifariki dunia akiwa njiani kupelekwa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Kahama kwa ajili ya kupatiwa matibabu baada ya kuvuja damu nyingi.

Hata hivyo, Kamanda huyo alisema jeshi hilo linawashikilia watuhumiwa wanane wakiwemo wanawake wanne waliokutwa wakiwa na Shotgun moja iliyokuwa imekatwa kitako na kuongeza kuwa majina yao wamehifadhiwa kwa uchunguzi zaidi.

Kamanda huyo alisema Polisi mkoani Shinyanga pia imekuwa katika mikakati ya kupambana na uhalifu tangu Novemba mwaka huu katika maeneo ya Wilaya ya Kahama na Shinyanga hasa maeneo ya Kakola, Tinde, Ulowa, Mwakitolyo na baadhi ya mitaa ya mjini hapa.

Alisema Polisi ilibaini kuwa baadhi ya watuhumiwa walioachiwa, na wengine waliotoka magerezani baada ya kumaliza vifungo vyao wanahusika zaidi na matukio ya uhalifu.

Pia alisema ufuatiliaji huo pia ulibaini kuwa baadhi ya wahalifu huwa wanahama pindi wanapoona maeneo waliopo si rafiki kwao na kuongeza kuwa wamewagundua baadhi ya wananchi waliokuwa wakitoa ushirikiano mkubwa kwa watuhumiwa hao na hatua zitachukuliwa dhidi yao.

Katika hatua nyingine, Polisi mkoani humo imesema itahakikisha inapambana vikali kumaliza masoko ya mali za wizi unaofanywa na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi kwa wananchi kwa lengo la kuweka mkoa huo salama.

Aliwaambia waandishi wa habari kuwa matukio ya uhalifu yamekithiri mkoani humo na wamebaini wafungwa walioachiwa ama kumaliza vifungo vyao wanahusika na uhalifu kwa kushirikiana na wananchi.


Asante sana kwa kutembelea Website hii Mungu akubariki sana


Karibuni sana

LINK CLASSIC

LIKE PAGE ZETU 




"KWA HABARI ZAIDI"

BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI

CODE HAPA

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply