UNGANA NA
LINK CLASSIC
KILA SIKU KWA HABARI MPYA
kuna sababu nyingi sana zinazoweza kuharibu mimba ya mama ikiwemo ugonjwa wa malaria, kaswende, kazi nyingi, magonjwa ya zinaa, u.t.i dawa fulani fulani mfano albendazole, misoprostol, metronidazole na kadhalika. lkiujumla sababu nyingi ambazo zinasababisha mimba kutoka huweza kuzuilika kwa kwenda kliniki mapema yaani pale tu unapohisi una mimba hata kama ni wiki mbili na kufuata ushauri wa wataalamu. sasa kuna wanawake wengi mimba zo huharibika na wao hushindwa kugundua mapema na matokeo yake anakaa na mtoto mfu hata miezi kadhaa bila kujua hivyo leo ntaongelea dalili za kuharibika kwa mimba kama ifuatavyo.
kutokwa na damu nyingi sehemu za siri; hii ni dalili kwamba mimba imeanza kuachia na mlango wa uzazi umeanza akufunguka sasa ukienda hospitali utakuta majibu mawili kwamba mtoto ameshafia tumboni au bado hajafa. lakini kama imeshatoka damu nyingi mtoto huyu atakufa tu.
mtoto kuacha kucheza tumboni; kwa kawaida mtoto huanza kucheza wiki ya 18 mpaka 20 kwa wanawake ambao hawajawahi kubeba mimba na wiki ya 16 mpaka 20 kwa wanawake ambao wamehsawahi kuzaa sasa ikitokea mtoto ameshawahi kucheza na sasa hachezi tena au muda huo umepitiliza na bado kimya kuna uwezekano mkubwa ameshafariki.
kupotea kwa dalili za ujauzito; mara nyingi mtu akipata ujauzito anakua na dalili nyingi kama kichefuchefu, kukosa hamu ya kula, kutapika sana na kubadilika sana tabia sasa zile dalili zote za mimba zikisimama ghafla basi ujue mimba imeharibika.
kuacha kuongezeka kwa mimba; tunategemea mimba kuendelea kua kubwa kulingana na umri unavyozidi kwenda mbele sasa kama mimba mara ya mwisho ilikua na miezi mitatu na leo ina miezi sita au mitano lakini iko haijabadilika ukubwa ujue mimba imeharibika.
maumivu makali ya tumbo; maumivu makali ya tumbo hasa kwa mimba kubwa sana au mimba ndogo sana kuna uwezekano mkubwa kondo imeanza kujiondoa kwenye kizazi kwa mimba kubwa au mimba ndogo imeshindwa kuendelea kukua. hii inaweza kua dalili kwamba mimba imeharibika.
kutoka kwa vipande vya nyama sehemu za siri; vipande vya nyama huashiria kwamba kuna mtoto anakua ameharibika tayari tumboni na mama kama huyu anatakiwa asafishwe kuondoa masalio yaliyobaki ili mama asiweze kupata madhara zaidi.
mwisho; kama nilivyosema mwanzoni mimba nyingi zinazoharibika hasa kwa nchi zetu za kiafrika hua kuna uzembe wa watu kutaka kujitibu wenyewe, kutokwenda kliniki mapema na kutofuata ushauri wa kitaalamu.
Asante sana kwa kutembelea Website hii Mungu akubariki sana
+255 (0) 652989873 – Whatsapp / Call
Karibuni sana
LINK CLASSIC
LIKE PAGE ZETU
"KWA
HABARI ZAIDI "
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: