sponsor

Slider

T - SHIRT PRINTING


LARGER FORMATING

STICKERS BRANDING | LARGE FORMATING


MIFUKO PRINTING

SMALL FORMATING

WEDDING | KITCHEN PART | SEND OFF | INVITATION CARDS

POSTERS | CARTOON | PHOTO PRINTING

» » » TANZANIA KUFUNGUA UBALOZI WAKE NCHINI QATAR KWA LENGO LA KUIMARISHA MAHUSIANO NA USHIRIKIANO

5be59f2c254a82bba089d96fd6648451

UNGANA NA
LINK CLASSIC
KILA SIKU KWA HABARI MPYA

Tanzania inatarajia kufungua Ubalozi wake nchini Qatar kwa lengo la kuendeleza na kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano kati ya nchi hizo huku ikitilia mkazo katika sekta za gesi asilia, utalii, usafiri wa anga na mawasiliano.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema hayo leo tarehe 16 Juni, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Qatar hapa nchini Mhe. Abdallah Jassim Al Maadadi.
Pamoja na kutangaza kuufungua Ubalozi wake nchini Qatar Dkt. Magufuli amemuomba Balozi huyo kufikisha ujumbe kwa Kiongozi wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani na Jumuiya ya wafanyabiashara wa Qatar kwamba zipo fursa nyingi za ushirikiano zinayoweza kufanyiwa kazi, huku akibainisha uwepo wa gesi asilia zaidi ya futi za ujazo Trilioni 57 na mpango wa kufufua shirika la ndege la taifa (ATCL).
“Najua Qatar ina uzoefu katika maeneo hayo na sisi Tanzania tungependa tushirikiane nanyi kuwekeza na kubadilishana uzoefu ili fursa hizo zilete manufaa kwa pande zote mbili” Amesema Rais Magufuli.
Kwa upande wake Balozi wa Qatar hapa nchini Mhe. Abdallah Jassim Al Maadadi amemshukuru Rais Magufuli kwa nia yake ya kufungua Ubalozi wa Tanzania nchini Qatar na kuimarisha zaidi ushirikiano na uhusiano na nchi hiyo, na amemuahidi kufikisha ujumbe kwa Kiongozi wa Qatar na Jumuiya ya wafanyabiashara wa nchi hiyo ili waje kuwekeza Tanzania.
aa3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Balozi wa Qatar hapa nchini  Mhe Abdallah Jassim Al Maadadi Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 16, 2016
MatataG_4336
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Qatar hapa nchini Mhe Abdallah Jassim Al Maadadi Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 16, 2016.
aaa5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiagana na Balozi wa Qatar hapa nchini Mhe Abdallah Jassim Al Maadadi baada ya kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 16, 2016.
Asante sana kwa kutembelea Website hii Mungu akubariki,
+255 (0) 652989873 Whatsapp / Call

Karibuni sana

LINK CLASSIC

LIKE PAGE ZETU 


KWA HABARI ZAIDI

BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI

CODE HAPA

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply