UNGANA NA
LINK CLASSIC
KILA SIKU KWA HABARI MPYA
Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro
amesema jeshi hilo linamuhitaji Askofu Josephat Gwajima wa
Kanisa la Ufufuo na Uzima kwa kuwa kuna mkanda wameupata
unaosemekana ni wake ambao unazungumza maneno ya
kichochezi.
Kamanda Sirro alisema: “Tumepata clip (mkanda) inayosemekama ni ya kwake. Tunamtaka athibitishe kama hayo maneno ni ya kwake. Na kama ni yeye ameyasema, anaelewa nini kuhusu kile alichokizungumza kwa sababu hayo maneno ni kichochezi. Tupo kwenye uchunguzi mama yangu.”
Jana, polisi jana walipiga kambi kwa saa saba kwenye geti la nyumba ya Askofu Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, wakitaka kumkamata bila ya mafanikio.
Polisi hao walikuwa kama wageni wa askofu huyo wakisubiri wafunguliwe geti, kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 10:10 jioni walipoamua kuondoka wakitumia gari aina ya Toyota Landcruser lenye namba za kiraia, ambalo kwa muda wote huo lilikuwa limeegeshwa pembeni mwa geti hilo.
Asante sana kwa kutembelea Website hii Mungu akubariki sana
+255 (0) 652989873 – Whatsapp / Call
Karibuni sana
LINK CLASSIC
LIKE PAGE ZETU
"KWA
HABARI ZAIDI "
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: