UNGANA NA
LINK CLASSIC
KILA SIKU KWA HABARI MPYA
Tumezoea kusikia au kushuhudia watu wanasema kwa kosa hili au tukio fulani ni unyanyasaji wa kijinsia bila kujua maana halisi na wala aina gani ya unyanyasaji wa kijinsia mtu amefanyiwa ikiwa amenyanyaswa kweli kijinsia.
Usiwe na hofu Kwani thelinkclassic.blogspot.com ipo na wewe karibu ili kuweza kukufahamisha nini maana ya unyanyasaji wa kijinsia na vilevile kujua aina zake na kujua kwanini watu hunyanyasa wenzao kijinsia na nini cha kufanya ili kuzuia unyanyasaji huo.
Unyanyasaji wa kijinsia ni kumdhalilisha mtu kwa sababu ya jinsia yake kwa kumpiga, kumbaka, kumbughudhi na kumnyang’anya kitu chochote ambacho ni haki yake,Kuna aina nyingi za unyanyasaji wa kijinsia kama Unyanyasaji wa Ngono,Unyanyasaji wa Kindoa, Unyanyasi nyumbani, Unyanyasaji wa Kitamaduni, Unyanyasaji wa Kisaikologia na vilevile unyanyasaji wa kingono kwa mtoto.
kwa kufahamu aina hizo za unyanyasaji, kwa pamoja tuone madhara ya unyanyasaji ni kama yafuatayo, Kudhurika kisaikologia na kimwili, kujenga chuki na jinsia iliyotenda unyanyasaji,Kuwa na hofu ya kudumu pale utapokumbuka unyanyasaji na kama muhanga wa unyanyasaji atakuwa amebakwa anakuwa ameumia kwa michubuko sehemu za siri,au kupata magonjwa ya kuambukizwa, kupata matatizo wakati wa kujifungua na wengine hupata fistula baada ya kushika mimba utotoni.
Sababu za unyanyasaji ni kutokuwa na usawa wa mahusiano kati ya wanaume na wanawake ambayo inasababisha Dhana ya wanaume kuonekana wana haki ya kutumia nguvu dhidi ya wanawake, dhana ya wanaume kuwa na mamlaka kwa wanawake hadi kuweka kutumia nguvu hata kwenye tendo la ndoa, wengine hudhani ni kawaida kumshika mwanamke sehemu za siri ni jamabo la kawaida, jamii kuwa na mawazo tofauti kwa mtu aliyefikwa na unyanyasaji wa kijinsia ni kujitakia na Mila na desturi ambazo zinachagiza unyanyasaji.
Nini kifanyike kuzuia unyanyasaji wa kijinsia ni kama ifuatavyo,Jamii inabidi ibadilishe mtazamo wa kuchukulia jambo kimazoea, Elimu kuhusu haki za wanawake na watoto, kutoa taarifa katika uongozi na jamii na serikali pale unaponyanyaswa au utakapoona kitendo cha unyanyasaji katika jamii inayokuzunguka.
Asante sana kwa kutembelea Website hii Mungu akubariki sana
+255 (0) 652989873 – Whatsapp / Call
Karibuni sana
LINK CLASSIC
LIKE PAGE ZETU
"KWA
HABARI ZAIDI "
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: