sponsor

Slider

T - SHIRT PRINTING


LARGER FORMATING

STICKERS BRANDING | LARGE FORMATING


MIFUKO PRINTING

SMALL FORMATING

WEDDING | KITCHEN PART | SEND OFF | INVITATION CARDS

POSTERS | CARTOON | PHOTO PRINTING

» » » CHANZO CHA HARUFU MBAYA UKENI


UNGANA NA 
LINK CLASSIC
KILA SIKU KWA HABARI MPYA

Hili limekuwa tatizo kwa wasichana na wanawake wengi hapa nchini Tanzania, bila kujua ni nini chanzo chake; kuna harufu ukeni ya kawaida kutokana na maumbile ya kibinadamu, uke una harufu yake lakini pale inapozidi ndio huwa tatizo.

Harufu ya ukeni ina sababu mbalimbali kama Dk. Hussein Ngaila kutoka Hospitali ya Salamana iliyopo maeneo ya Temeke, Jijini Dar es Salaam, anasema kuna kuwashwa, kutokwa na uchafu na kuungua, lakini anaongezea kuwa harufu ya ukeni inabadilika kutokana na mzunguko wa hedhi wa mwanamke na inasikika pale mwanamke anapokuwa anashiriki tendo la ndoa.

Nini sababu ya mwanamke kutokwa na harufu kali ukeni?

Bacteria

Kwa kawaida kwenye sehemu za siri za mwananke huwa kuna bakteria, inapotokea mwanamke anakuwa na bakteria wengi ukeni inamsababishia kuwa na harufu kali ukeni.

Uchafu

Jinsi ya kusafisha sehemu za siri ni ujuzi, lakini Dk. Hussein anasema kuwa unaposhindwa kujisafisha vizuri unajisababishia harufu kali ndani ya uke.

gonjwa ya zinaa

Kutokana na magonjwa ya zinaa kama kaswende na mengineyo husababisha mwanamke kutokwa na harafu ukeni.

 Mabaki ya pedi

Dk. Hussein anasema kuwa pale mwanamke anapokuwa kwenye dedhi  na kushindwa kujitunza na kuacha mabaki ya uchafu ukeni yakioza kwa kiasi kikubwa husababisha harufu kali ukeni.

Festitula

Ni hali ya muunganiko  katika kutoa uchafu wa mwili unaosababishwa na tundu linalotokea wakati mwanamke anapojifungua katika misuli kati ya uke na kibofu cha mkojo au kati ya uke na njia ya haja kubwa au vyote viwili na kusababisha harufu kali ukeni.

Magonjwa sugu kama saratani ya kizazi

Kutokana na wimbi kubwa la ugonjwa wa saratani hasa kwa wanawake hupelekea matatizo mbalimbali lakini hasa pale inapofikia hatua ya kuleta harufu hasa kwa wale waliopata maambukizo ya saratani.

Kwa Mujibu wa Dk. Ngaila anasisitiza mwanamke anapogundua dalili hizi hana budi kuwahi hospitali kwa ushauri  na vipimo ili kubaini tatizo kwa kutokomeza hali hii ya unyonge kwa wanawake na wasichana.

Asante sana kwa kutembelea Website hii Mungu akubariki sana
+255 (0) 652989873 – Whatsapp / Call

Karibuni sana
LINK CLASSIC

LIKE PAGE ZETU 



"KWA HABARI ZAIDI "

BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI

CODE HAPA

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply