UNGANA NA
LINK CLASSIC
KILA SIKU KWA HABARI MPYA
Waislam wakiwa katika kumi la pili kumi la TOBA wanahusiwa kuomba msamaha kwa mola wao dhidi ya yale yote waliyo yafanya mwaka uliopita na wasiendelee nayo tena maishani mwao, hiyo ndio Toba inakubalika kwa Mwenyezi Mungu, ila yeye ndiye mjuzi zaidi.
NINI MAANA YA TOBA?
Toba maana yake kukiri na kujutia makosa yako yote uliyowahi kuyafanya na kumuomba Allah (Mungu) kuwa hutorudia tena katika maisha yako. Ukiyafanya hayo na kuyaacha moja kwa moja pasina kurudia Allah S.W atakuwa amekusamehe na atakuongezea Darja kwa maana ya kuwa na nafasi ya kipekee kwake.
FADHILA NA MALIPO ZA IBADA NDANI YA MWEZI KTUKUFU WA RAMADHANI.
Mwenyezi Mungu ameahidi kuwa unapofanya ibada ya Faradh(ibada ya lazima) malipo yake sawa na Darja 70 wakati ukifanya Sunna malipo yake sawa na malipo ya miezi ya kawaida. Utajiuliza malipo ya miezi ya kawaida ni ngapi kwa Faradhi moja? malipo ya miezi ya kawaida kwa faradhi moja Darja 25 hadi 27 .
MAJUMUISHO YA MALIPO KWA SIKU
Endapo utatekeleza ibada ya swala tano kwa siku na malipo ya faradhi moja kwa mwezi huu ni 70 ukijumulisha kwa vipindi 5 unapata DARJA 350. Ukifanya sunna mbalimbali mfano umewahi asubuhi umeswali q-bria, adhuhuri umeswali q-bria na baadia laasir q-bria magharib q-bria na Baadia al ishai q-bria na baadia unapata Darja 200 hapo hatuja hesabu Sunna nyingine tofauti tofauti mfano Taraweeh na nyiradi mbalimbali. Hujachelewa anza sasa ili uvune malipo yaliyokuwa makubwa maana mwezi wa Ramadhan upo ila binadamu hana uhakika na pumzi yake.
Asante sana kwa kutembelea Website hii Mungu akubariki sana
+255 (0) 652989873 – Whatsapp / Call
Karibuni sana
LINK CLASSIC
LIKE PAGE ZETU
"KWA
HABARI ZAIDI "
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: