UNGANA NA
LINK CLASSIC
KATIKA KIPENGELE CHA
HOT NEWZ
Seriikali imesema kwamba haitawalipa watu wote ambao wamebomolewa nyumba zao kwa kujenga mabondeni au kujenga maeneo ya wazi,hifadhi ya barabara, au maeneo yaliyotengwa kwa shughuli maalumu.
Hayo yameelezwa Bungeni na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi. Angelina Mabula wakati akijibu swali la Mbunge wa Wingwi Kisiwani Zanzibar Juma Kombo Hamad ambaye ametaka kujua ni lini serikali itawalipa fidia wananchi ambao wamevunjiwa nyumba zao bila ya serikali kuwalipa kwani wakati wakijenga serikali iliwaona na kukaa kimya.
Akijibu swali hilo Naibu Waziri Mabula amesema kwa mujibu wa sheria ya mazingira ya mwaka 2004 na sheria ya mipango miji ya mwaka 2007 inaweka bayana sehemu ambazo wananchi hawatakiwi kujenga ikiwemo maeneo oevu, mabondeni, na vyanzo vya maji ambapo mwananchi akitaka kujenga ni lazima ajenge umbali wa mita 60 maeneo hayo.
Bi. Mabula ameongeza kuwa kutokana na wananchi kukiuka maagizo hayo serikali haitawalipa fidia hivyo ni wajibu wa wananchi kufuata sheria za nchi ili kuepuka migongano isiyo ya lazima.
Aidha Bi. Mabula amezitaka halmashauri zote nchini kuwa makini katika kusimamia sheria kwani imebainika kuwa nyumba nyingi huwekwa alama ya X na halmashauri lakini ufuatiliaji unakuwa haupo ndiyo maana matatizo hayo yamekuwa yakijirudia.
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: