UNGANA NA
LINK CLASSIC
KATIKA KIPENGELE CHA
HOT NEWZ
Shirikisho la wenye Viwanda nchini Tanzania (CTI) limeiomba serikali kuchukua hatua dhidi ya wafanyabiashara wachache wanaokiuka taratibu za vibali vya uingizaji sukari kutoka nje ya nchi ili wasiumize sekta ya viwanda nchini.
Shirikisho hilo limefikia hatua hiyo ya kuiomba serikali kuwachukulia hatua wafanyabiashara wachache wanaokiuka taratibu badala ya kuja na utaratibu unaowaumiza wafanyabiashara waadilifu kiasi cha kutishia ukuaji wa sekta ya viwanda nchini.
Mwenyekiti wa CTI Samuel Nyantahe, ametoa ombi hilo Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa mwaka wa wanachama wa CTI, mkutano uliokuwa unajadili mustakabali wa sekta ya viwanda na hasa jinsi wamiliki hao wanavyoweza kushirikiana na serikali katika kufanya ndoto ya Tanzania ya Viwanda ikatimia.
Akizungumza kwa niaba ya mgeni rasmi Waziri wa Viwanda na Biashara, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maeneo Huru ya Uwekezaji EPZA, Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia, amesema serikali inashirikiana kwa karibu na sekta binafsi kuhakikisha kunakuwa na mazingira rafiki kwa ajili ya uanzishwaji wa viwanda vingi na hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi.
LINK CLASSIC: Asante sana kwa
kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia
endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya
Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea
website hii
Pia
waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
+255
(0) 652989873 whatsapp
Karibu sana
LINK CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: