UNGANA NA
LINK CLASSIC
KATIKA KIPENGELE CHA
HOT NEWZ
Asilimia 80 ya uchumi wa Tanzania unategemea sekta ya kilimo kama chanzo kikubwa cha mapato yake, pamoja na hayo serikali imeendeleza jitihada zake za kuwakwamua wakulima kwa kutenga fungu la kutosha ili kuhakikisha sekta hiyo inazidi kukua na kuendelea kuwa msaada mkubwa kwa Watanzania.
Pamoja na jitihada hizo kumekuwepo na changamoto kadha wa kadha kwa wakulima hali inayoifanya Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini kuingilia kati ili kupatia ufumbuzi changamoto zilizopo huku ikiwataka wakulima kuunda vikundi ili waweze kupatiwa mikopo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mapema leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo, Thomas Samkyi amesema ukosefu wa taarifa za mauzo ya mazao kwa baadhi ya wakulima ili kuweza kupatiwa mikopo imekuwa ni kikwazo kikubwa kinachowakwamisha wakulima wengi.
“Wakulima wengi hawana taarifa sahihi za mapato zinazotokana na mazao hali inayosababisha taasisi nyingi za kifedha kushindwa kuwapatia mikopo kwa wakulima” Alisema Samkyi .
Samkyi amesema kutojihusisha kwa wakulima katika vikundi ili kupatiwa mikopo imekuwa kikwazo kikubwa kwa wakulima hao kuweza kupatiwa mikopo yenye masharti nafuu kutokana na kuweka dhamana ya nyumba zisizo na ubora ili kupatiwa mikopo hiyo hali inayochangia kunyimwa mikopo katika taasisi za fedha.
“Wakulima wengi wamekuwa na nyumba ambazo hazina ubora wala hati hali inayochangia wakulima wengi kutoweza kupatiwa mikopo” aliongeza Samkyi.
LINK CLASSIC: Asante sana kwa
kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia
endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya
Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea
website hii
Pia
waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
+255
(0) 652989873 whatsapp
Karibu sana
LINK CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: