Imeelezwa kuwa Serikali haina mamlaka ya kuamrisha waajiri katika sekta binafsi kulipa wafanyakazi wao mishahara kama ilivyoainishwa na serikali kwani huwa ni makubaliano baina ya mwajiri na mwajiriwa.
Hayo yamejiri mara baadaya Tamko lililotolewa na Mwenyekiti wa chama cha madereva wa mabasi nchini Shaban Mdemu kuwa hawajaridhishwa na tamko lililotolewa na kamati ya kudumu iliyoundwa mwaka jana mara baadaya mgomo wa madereva nchi nzima iliyowasilishwa na Katibu mkuu Wizara ya Kazi na Ajira Erick Shitindi.
Bwana Shitindi amewasilisha tamko hilo mapema leo jijini Dar es salaam mbele ya wanahabari ambapo amesema kuwa jukumu lao kama serikali ni kuhakikisha wanasimamia madereva kupewa mikataba ya kudumu ila kwa suala ya mishahara na posho litabaki kuwa makubaliano kati ya mwajiri na mwajiriwa.
“Serikali haina mamlaka ya kuamrisha mwajiri alipe waajiriwa wake kwani hayo hubaki makubaliano binafsi kati ya mtu na mtu tunaweza kumpangia afu asiwe na uwezo na kiwango kile hivyo sisi tunahakikisha unapata mkataba unaotambulika na Serikali ili kulinda haki zako ila mshahara na posho zitabaki makubaliano binafsi”. Alisema Shitindi
Mnamo tarehe 09 -04-2015 ulifanyika mgomo wa madereva nchi nzima uliohusu malalamiko na kero mbalimbali za madereva katika kuzipatia ufumbuzi kero hizo aliyekuwa waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Kayanza Pinda, aliunda Kamati ya kudumu ya kutatua kero na Changamoto mbalimbali katika Sekta ya Usafirishaji.
LINK CLASSIC: Asante sana kwa
kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia
endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya
Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea
website hii
Pia
waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
+255
(0) 652989873 whatsapp
Karibu sana
LINK CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: