UGONJWA wa kipindupindu umeendelea kuwatesa wananchi baada ya watu 320 kupoteza maisha huku watu 20,294 ,wameugua ugonjwa huo tangu uanze Agosti 15 mwaka jana.
Katika mazungumzo yake na vyombo vya habari jijini Dar es Saam Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alieleza kuwa kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka ,mwenendo wa ugonjwa huo unaashiria idadi ya wagonjwa inazidi kuongezeka nchini.
Mwalimu almesema Januari kulikuwa na wagonjwa 2,272 na Machi kulikuwa na wagonjwa 2,956 na kwamba hilo ni ongezeko la asilimia 30.1.
“Baadhi ya mikoa imeonesha uendelevu wa kupungua kwa idadi ya wagonjwa wa Kipindupindu kwa robo ya kwanza ambayo mikoa hiyo ni Simiyu, Rukwa na Mbeya, takwimu hizi za nchi nzima zinaashiria kuwa juhudi za kupambana na ugonjwa huo zinahitajika kutekelezwa na kusimamiwa kikamilifu katika mikoa yote,” alisema Mwalimu.
Mwalimu alisema kipindi cha Machi wagonjwa wapya walioripotiwa nchi nzima walikua 2,956 na na vifo 53.
Amesema Machi 5 hadi April 3 zinaonyesha idadi ya wagonjwa imeongezeka kwa asilimia 59.5 ikilinganishwa na idadi ya wagonjwa February walikua 1,853 hata hivyo mikoa ya Tanga,Pwani na Mtwara haikuwa imeripoti wagonjwa mwezi wa Februali lakini Machi imepata wagonjwa wapya.
“Kumekuwa na ongezeko kubwa la wagonjwa wapya kwenye Mikoa ya Geita, Kilimanjaro, Manyara, Morogoro,na Dodoma katika kipindi cha mwezi mmoja na wagonjwa kutoka mikoa ya Simiyu,Mbeya na Iringa imepungua kati ya Februari na Machi mwaka huu,” alisema Mwalimu.
Mwalimu amesema kwa upande wa takwimu za kila siku idadi ya wagonjwa walioripotiwa kati ya Machi 28 na Aprili 2016 imepungua kwa asilimia 37.2 ikilinganishwa na wagonjwa walioripotiwa Machi 21 hadi 17 mwaka huu.
LINK CLASSIC: Asante sana kwa
kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia
endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya
Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea
website hii
Pia
waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
+255
(0) 652989873 whatsapp
Karibu sana
LINK CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: