Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Bradley Gordon, alitoa taarifa hiyo kwenye mawasiliano na wafanyakazi wa kampuni hiyo. Alisema kutokana na makadirio, kampuni hiyo italipa kodi ya ushirika ya miaka mitatu, endapo kampuni hiyo mwaka huu itaingiza mapato yanayofikia kiasi cha dola za Marekani milioni 80.
Alisema mkataba kati ya Acacia na TRA umetiwa saini na umetambuliwa na pande zote mbili kwamba hakuna kodi yoyote ya mapato yatokanayo na faida ambayo Acacia inastahili kulipa, haitalipwa.
Gordon alisema Acacia Mining ambayo iliingia nchini katika sekta ya madini ikijulikana kama Barrick na baadaye kama African Barrick Gold miaka 15 iliyopita, imekuwa ikitengeneza faida lakini haijarejesha mtaji iliowekeza wa dola za Kimarekani bilioni 3.8.
Hivi karibuni, Baraza la Rufaa za Kodi (TRAT), liliamua katika rufaa iliyokatwa na Acacia kwamba kampuni hiyo ilijenga mazingira ya kukwepa kodi ya dola za Marekani 41,250,426 (Sh bilioni 89) kwa kipindi cha miaka minne mfululizo.
LINK CLASSIC: Asante sana kwa
kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia
endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya
Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea
website hii
Pia
waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
+255
(0) 652989873 whatsapp
Karibu sana
LINK CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: