WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa mita mpya za kupimia mafuta (Floor Meter) na kuagiza Mamlaka ya Bandari (TPA), kuhakikisha inaweka wataalamu watakaosimamia vizuri mita hizo.
Alisema, mita hizo mpya zitaiwezesha mamlaka hiyo kupata vipimo sahihi vya mafuta na kukusanya mapato yanayostahili, kulingana na mafuta yaliyopo.
Akizungumza alipofanya ziara kukagua mita hizo zinazojengwa Kigamboni, Dar es Salaam, Profesa Mbarawa alisema kuwa zimekwishaanza kufanyiwa majaribio na zitaanza kufanya kazi Mei. “Nawaagiza muajiri wataalamu wa kusimamia hizi mita ili kuziwezesha kufanya kazi kikamilifu. Ujenzi wake unagharimu Sh bil 12,” alisema Profesa Mbarawa.
Alitembea daraja jipya la Kigamboni aliloeleza kuwa litazinduliwa Aprili 16, mwaka huu na Rais John Magufuli na kuwataka wananchi wa maeneo hayo kutoharibu miundombinu ya daraja hilo. Katika hatua nyingine, Mbarawa alitembelea eneo la kusafirishia mizigo inayokwenda Zanzibar na kuagiza mazingira ya kazi ya eneo hilo yaboreshwe.
Pia, alisisitiza umuhimu wa kuboresha huduma za benki ili kuondoa adha ya wafanyabiashara kusafiri na fedha kwa umbali mrefu kwani ni hatari kwa usalama wao. “Mamlaka ya Bandari inatakiwa kuweka mifumo ya kielektroniki katika utendaji kazi zake, acheni kutumia karatasi,” alisema.
LINK CLASSIC: Asante sana kwa
kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia
endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya
Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea
website hii
Pia
waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
+255
(0) 652989873 whatsapp
Karibu sana
LINK CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: