Ungana na LINK CLASSIC katika kipengele cha
ELIMU YA AFYA ZETU
topic ni
MADAKTARI BINGWA WA VICHWA WAKO 8 NCHI NZIMA
Katika Kuokoa maisha ya Mtanzania anaepata matatizo yanayohitaji Upasuaji wa kichwa na mishipa ya fahamu Serikali kupitia wizara ya Afya kwa kushirikiana na Taasisi ya Mifupa MOI imefungua kozi ya upasuaji wa vichwa na mishipa ya Fahamu ili kuongeza madaktari wenye fani hiyo, kwani hadi sasa kuna madaktari nane pekee Nchi nzima.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ambapo ameainisha kuwa Tanzania ina madaktari nane pekee wanaohusika na Upasuaji wa vichwa na mishipa ya Fahamu ambapo saba kati yao wapo Hospitali ya Taifa Muhimbili kitengo cha Upasuaji wa Mifupa (MOI) na mmoja yupo Bugando Mwanza.

“Wizara imeanzisha kozi kwa ajili ya kuongeza wataalamu wengi zaidi kwani hadi sasa tuna madaktari nane pekee ambapo saba kati yao wapo MOI na mmoja hospitali ya Rufaa ya Bugando Jijini Mwanza”.Alisema Ummy
Waziri Ummy amewataka madaktari hao kuzunguka nchi nzima kwa ziara watakayojipangia kwa mwaka mzima waweze kuwafikia hata wasiokuwa na uwezo wa kuwafika Muhimbili na Mwanza.
LINK CLASSIC: Asante sana kwa
kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia
endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya
Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea
website hii
Pia
waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
+255
(0) 652989873 whatsapp
Karibu sana
LINK CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: