Ungana
na LINK CLASSIC katika kipengele
cha
ELIMU YA AFYA ZETU
topic ni
ZIJUE SABABU ZA MIMBA KUHARIBIKA SOMA ZIKO HAPA
Kuharibika kwa mimba ni hali ya mwanamke kupata ujauzito na
ukatoka kabla ya muda wake ambapo tatizo hili huangaliwa kabla
ya kutimiza wiki 20 tangu kutungwa kwake.Hali hiyo inapotokea
huitwa kuwa mimba imetoka au imeharibika (Miscarriage).
Hali hii ya mimba kuharibika inakuwa tofauti kabisa na utoaji
mimba ambapo kitendo cha kutoa mimba kinafanywa na binadamu
kwa makusudi na huwa amedhamiria kufanya hivyo.
Akielezea tatizo la mimba kuharibika Daktari Msaidizi w
a Kituo cha Afya Nkwenda Wilayani Karagwe, Dk Aristides
Ruhikula anasema kuwa katika hali hiyo mtoto anakuwa hawezi
kujitegemea mwenyewe kwa mahitaji yanayotakiwa ikiwa ni
pamoja na kupumua, hivyo hali hiyo ya kutojitegemea husababisha
kifo.
Sababu za mimba kutoka
Anasema kuwa miongoni mwa sababu zinazosababisha mimba
kutoka ni pamoja na umri mkubwa ambapo kwa kawaida
mwanamke anapofikisha umri wa miaka 35 au zaidi
misuli(sphencters) ya mji wa uzazi hulegea na kupunguza nguvu za
kuweza kuhimili na kutunza kiumbe kinachokuwa ndani ya mji
wa uzazi, hivyo kusababisha mimba kutoka.
Hitilafu katika kizazi ambayo huwa katika mfuko wa
mimba(uterus) ambao muundo wake siyo wa kawaida.Wanawake
wenye tatizo kama hili huwa na hatari kubwa ya mimba kuharibika
kabla ya miezi tisa.
Aidha maambukizi ya fangasi au bakteria husababisha misuli ya
kizazi kushambuliwa hivyo kupoteza uwezo wake wa kuhifadhi
ujauzito hivyo mimba kuharibika. Miongoni mwa sababu
zinazosababisha mimba kuharibika ni matatizo ya vinasaba(genetic
factors)
Hali hiyo hutokana na hitilafu katika kromosomu(cromosomal
abnormalities) ambayo husababisha vinasaba kuwa katika hali isiyo
ya kawaida ambayo hali hiyo ni miongoni mwa sababu kubwa
zinazosababisha mimba kutoka kabla ya kutimiza wiki 13.
Hii husababisha damu ya mama kushindwa kuendana na damu ya
mtoto hivyo kutokea kwa madhara ambayo humdhuru mtoto na
kumfanya ashindwe kuhimili hali ya tumboni kwa mama hivyo
kutoka nje.
Pia ukosefu wa homoni ya progesterone ambayo hufanya kazi
kubwa tangu kutungwa kwa mimba hadi mtoto kuzaliwa ambayo
huchochea uimara wa ukuta wa placenta ambao mtoto hujishikiza.
Upungufu wa homoni hii husababisha ukuta wa mji wa mimba
kushindwa kuhimili uzito wa mtoto, hali ambayo husababisha
ujauzito kuharibika kabla ya muda wake.
Sababu nyingine ni utumiaji wa pombe kali, sigara na dawa za
kulevya. Utumiaji wa vitu hivi huchangia mimba kutoka kutokana
na kemikali nyingi zilizomo. Hivyo mwanamke mjamzito
hushauriwa kutotumia vitu vyenye kemikali, ili kulinda afya yake
na mtoto aliyeko tumboni.
Pia baadhi ya vyakula na vipodozi huwa vina kemikali ambazo
hupelekea shingo ya kizazi kulegea na kadiri mimba inavyozidi
kukua huendelea kuachia na kusababisha mimba kushuka,hali
inayosababisha mimba kuharibika.
Dalili za mimba kuharibika(symptoms of a miscarriage)
Dk Ruhikula anaeleza kuwa dalili zinazojitokeza wakati wa
mimba kuharibika ni pamoja na kutokwa na damu sehemu za siri.
Hiyo ni dalili kubwa ya mimba kuharibika ambapo damu hiyo
hutoka sawa na mwanamke anayekuwa kwenye siku zake.
Maumivu katika viungo ambayo huwa makali katika kiuno, nyonga
na tumbo chini ya kitovu ambapo maumivu hayo huanza taratibu,
lakini huongezeka kadiri muda unavyozidi kusonga mbele ambapo
hali hiyo huambatana na kutokwa damu sehemu za siri.
Dalili nyingine ni kutokwa na uchafu sehemu za siri. Hii ni dalili
kubwa ya mimba kutoka. Mama mjamzito kuanza kutokwa na
uchafu mwingi wenye rangi sambamba na mabonge ya damu.
Kupata maumivu ya kiuno huku ukisikia maumivu hayo yanashuka
chini kwa nguvu fahamu fika mimba yako inaweza kutoka muda
wowote.
Madhara yatokanayo na kuharibika kwa mimba
Iwapo mama mjamzito amepata tatizo hili na hajapata tiba sahihi kama kuna mabaki tumboni yanaweza kusababisha madhara mengine ikiwemo kizazi kuoza au kusababisha matatizo mengine kwenye mji wa mimba.
Miongoni mwa madhara yanayoweza kumpata mama ambaye mimba imeharibika ni pamoja na kizazi kuharibika ikiwa mama hatasafishwa vizuri tumboni baada ya mimba kuharibika.
Madhara mengine ni kuugua mfululizo baada ya ujauzito kuharibika pamoja na kushambuliwa na madhara mfululizo baada ya ujauzito kuharibika.
Pia mama anaweza kupata madhara ya kisaikolojia ambayo yanachukua muda mrefu kusahaulika hasa pale wanapokutana na wanawake wajawazito au wenye watoto.
Matibabu
Mwanamke mwenye tatizo la kuharibika kwa mimba anaweza
kupata matibabu kwa njia mbalimbali kutegemea na mgonjwa
husika.
Matibabu hayo hupatikana hospitalini ambapo mwanamke
anatakiwa kuwahi pale anapoona dalili hatarishi.
Kwa yule mwenye historia ya kuharibika kwa mimba na tayari ana
mimba atapata matibabu tofauti na yule mwenye tatizo hilo, lakini hana mimba kwa muda huo.
Ushauri
Dk anasema kuwa dalili zilizotajwa hapo juu peke yake hazitoshi
kuonyesha kuwa mimba imeharibika bali mama mjamzito
anapoona dalili moja kati ya hizi au zote hata hali ambayo haielewi
anatakiwa kuwahi hospitalini ili kuweza kupata vipimo.
Endapo mama huyo atachelewa atakuwa anajiweka katika hali
mbaya kutokana na sumu inayotokana na kiumbe kilichoharibika
na kusababisha matatizo kwenye mfuko wa uzazi ikiwemo
ugumba.
Mwanamke yeyote ambaye hajapata tatizo hilo anashauriwa kula
vyakula kama maboga, mboga za majani na vyakula vyote
vinavyojenga mwili.Pia wanatakiwa kuacha matumizi ya vipodozi
vyenye kemikali pamoja na uvutaji wa sigara na dawa za kulevya
ili kujikinga na tatizo la kuharibika kwa mimba
LINK CLASSIC: Asante sana kwa
kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia
endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya
Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea
website hii
Pia
waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
Karibu sana
LINK CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: